Saturday, December 23, 2017

DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir:

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk.Edmund Mndolwa amesema ndani ya siku 100 kuanzia jana atahakikisha analipa madeni yote wanayodai watendaki wa jumuiya hiyo huku akitoa onyo kwa wale wenye tabia ya kutengeneza makundi.

Amesema hayo wakati anazungumza na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kumpokea rasmi ambapo amesisitiza kusimamia vema majukumu yake kwa maslahi ya jumuiya na CCM kwa ujumla.

Kuhusu madeni,amesema anatambua changamoto zilizopo ikiwamo ya watendaji wa ngazi mbalimbali kudai fedha zao lakini hilo atalishughulikia ndani ya siku 100 kwani fedha zipo."Najua changamoto zilizopo kwenye jumuiya yetu,nitumie nafasi kuwahakikishia watendaji wanaodai ndani ya siku 100 tutalipa madeni yote.

" Nitaboresha maslahi na kubwa zaidi tutanunua vitendea kazi kwani vilivyopo vimechakaa na viachache.Lengo na kuifanya jumuiya yetu kutimiza majukunu yake na tutaendelea kujiimarisha hatua kwa hatua,"amesema.Ametumia nafasi hiyo kuelezea kusikitishwa kwake na tabia ya uwepo wa makundi ambayo kimsingi hayana nia njema zaidi ya  kukiharibu chama chao ,hivyo lazima wakomeshe makundi .

"Atakayebainika anajihusisha na makundi atachukuliwa hatua,sisi ni wamoja na lazima tusimame katika hilo.Chaguzi zimekwisha ndani ya jumuiya ,sasa tufanye kazi," amesema Dk.Mndolwa.Ametoa onyo kuhusu tabia ya watu kuwa na tabia ya kuzungumzia mambo ya jumuiya na chama bila kufuata utaratibu.

Hivyo amesema lazima anayetaka kuzungumza basi ahakikishe anatumia vikao halali ambapo atajenga hoja na kusikilizwa."Atakayezungumza bila kufuata utaratibu hatutamuacha,lazima kanuni na taratibu ziheshimiwe na kila mmoja wetu,"amesisitiza.

Akizungumzia uchumi,ameweka wazi atatumia elimu yake na maarifa yote kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzisha vitega uchumi na vilovyopo kuvisimamia imara ili viwe na tija.Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam ,Frank Kamugisha amempongeza Dk.Mndolwa na kuitumia nafas hiyo kueleza mipango ya kimaendeleo ambayo wampanga kuifanya.

Baadhi ya mipango ya jumuiya ya wazazi Dar es Salaam ni kuanzisha Saccos na azma yao ni kuwa na benki ya wazazi ambapo amesema kila kitu kinakwenda vizuri na wanachokizungumza si porojo.Pia amesema wanaomkakati wa kuwa na kiwanda ambacho kitakuwa kinazalisha sare na Aprili mwakani timu ya wataalam itakwenda Afrika Kusini ambako lina kiwanda cha kutengeneza sare kujifunza na baada ya hapo watakwenda China kuangalia bei ya mitambo.

"Haya ambayo tunakueleza mwenyekiti wetu tumejipanga na tunadhamira ya kweli ya kuleta maendeleo katika jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam.Tunaomba tu ushirikiano wenu tutakapopiga hodi mtupokee," amesema Kamugisha.

Wakati huo aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Wananchi(FUC)Omari Kimbau ameamua kujiunga CCM.

Amesema  sababu kubwa ni kwamba haoni sababu ya kuwa mpinzani wakati Rais John Magufuli anafanya kazi nzuri kiasi cha wapinzani kutokuwa na ajenda tena.

No comments:

Post a Comment