Na David John
BAADHI ya wanachama wa Shirikisho la waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) wamewajia juu viongozi wa Shirikisho huku wakihoji uhalali wao wa kuendelea kufanya kazi.
Wamesema kuwa viongozi hao muda wao wa kuongoza ulishapita na wanachama walishatoa msimamo wa kuwataka kujiudhuru ili kupisha kufanyika kwa uchaguzi mwaka kesho.
Akizungumza kwa niaba ya wezake mmoja wa wanachama hao Rajabu Hassan amesema wamepata taarifa kwamba kuna baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo wamekwenda mjini Dodoma kusimamia uchaguzi wa shirikisho vyama kwa ngazi ya mkoa kinyume cha taratibu.
Amesema maamuzi ya Halmashauri kuu ya shirikisho hilo ilikuwa kuwa chaguzi zote ambazo zitafanyika ngazi za wilaya na mikoa zisimamiwe na wajumbe wa halmashauri kuu na si viongozi wakuu na hiyo nikutokana wao walipewa kuendesha shirikisho kwa muda ambapo muda wao umekwisha kimsingi.
“unajuwa ndugu mwandishi kimsingi viongoza hawa hawana Sifa na kinachosubiliwa na mkutano mkuu na Hata hivyo mwenyekiti anakwenda yeye pekee yake kinyume na katiba kwani kila kitu anakwenda kufanya yeye. “Amesema Hassan
Nakuongeza kuwa pia mwenyekiti huyo amekuwa mbabe kwani ikitokea mwanachama anahoji jambo basi anatishia kumfutia uwanachama pamoja na kumuondoa kwenye makundi yao ya mawasiliano.
Naye mwanachama mwingine kwa sharti la kutotaja jina lake amesema wanajuwa mchezo unaofanyika na viongozi hao nikutaka kujitengenezea mazingira ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu ujao uliopangwa kufanyika ndani ya shirikisho hilo mwakani.
Mmoja wa wataalamu wa Tiba hiyo ya dawa asili nchini akizungumzia hatua ya viongozi hao kuendelea kufanya kazi amesema kimsingi hadi sasa hakuna shirikisho na linasemewa mtaani tu.
” Kisheria hakuna chombo kinachoitwa shirikisho kwani uhalali wake ulishapita na hata kinachofanyika ndani ya shirikisho kwa sasa ni batili. “amesema.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili nchini Richrd Kayombo amesema mambo yanayoendelea ndani ya shirikisho hilo ni ya kwao wao kama Baraza wanafanya kazi na mganga mmoja mmoja.
Awali waliwataka watengeneze chombo kitakachowazungumzia mambo yao lakini mambo yanayofanyika wanajuwa wenyewe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho hilo Abdallahman Lutenga amewataka wanachama wake kutambua kuwa shirikisho ni mahala patakatifu hakuna mchwa wala nani atakayeingia hapo.
Amesem yeye anamamlaka ya kusimamia chaguzi kwani ndio rais wa shirikisho lakini ndio anaye teua na kuitisha mikutano ya shirikisho hilo.
” Nataka nikuambie kwanza wakati mwingine muwe mnauliza kwanza huko chini kabla ya kuja kwangu kwani mimi ni kiongozi mkubwa na nina kazi nyingi na anatambulika na Serikali. “amesema
Hassan Rajabu mmoja mwanachama wa shirikisho la vyama vya waganga wa tiba asili Tanzani.
Shirikisho nimefanya kazi na SERIKALI na uongozi uliopo upo kwa mujibu wa katiba.
ReplyDeletena mwenyekiti wake ndiye msemaji na ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na kusimamia uwekaji wa viongozi wa mikoa na wilaya. hakuna kifungu chochote cha katiba kinachowapa mamlaka wajumbe wa halmashauri kuu kufanya kazi za mwenyekiti wa taifa au kamati tendaji.
pia shirikisho halina mwanachama anaeitwa HASSAN RAJABU sisi tunamshangaa huyo mtu wala hatujui alikotokea.zaidi ya kuwa ni mtumwa wa vurugu tu.
pia msajili wa mambo ya ndani ndiye anaejua UKWELI viongozi waliopo madarakani kama muda wao umeisha au la. mwenyekiti wa baraza la tiba asili siyo msemaji wa shirikisho wala jana mamlaka yoyote na shirikisho ndiyo maana ametoa majibu ya kitoto yasiyo na mizania .
Sahihi kabisaa anachokiongeaa kiongozii hapo.na huyuu ndugu anayesema shirikishi halipo ni muhongo na hana ushahidii wowote wa kuthibitisha kuwa shirikisho halipo kwani kipindii cha uongozii wao hao wakina rajabu kipindi akiwa mwwnyekiti katika wilaya ilala ndo walishindwa kuonesha uwpo wao kama viongozii ili kulifanya shilikisho kuwa na nguvuu sasa tuwambiee tuu tumekuja
ReplyDeleteVijana wa kazi katika
Shirikishoo
Tunatala sasa kulipa nguvunshirikishoo litambulike
Na liheshumikee ahsanteni