Tuesday, November 28, 2017

Vijana Dar watunukiwa vyeti baada ya kuhitimi masomo ya ufundi kupitia VSOMO

 Mamlaka ya mafunzo ya ufundi VETA leo imekabidhi vyeti vya kuhitimu masomo ya ufundi stadi kwa vijana 8 wa mkoa wa Dar es saalam baada ya  kuhitimu masomo yao ya ufundi wa umeme wa majumbani pamoja na ufundi wa simu mara baada ya kumaliza kusoma kupitia aplikesheni  ya VSOMO na kuhitimu katika viwango vya VETA.
 Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es saalam , Habibu Bukko aliishukuru  Airtel kwa ushirikiano wake na VETA kupitia  Aplikesheni ya VSOMO ambapo imekuwa ikifaidisha wanafunzi walioko mbali na vyuo vya VETA kuweza kusoma VETA wakiwa popote, vilevile alipongeza vijana hao kwa kutumia simu zao za mkonononi vyema na kuhitimu masomo ya  ufundi
 Alisema jitihada hizi za Kufanikiwa kutoa Masomo ya Ufundi stadi kupitia Aplikesheni ya VSOMO zinaenda sambamba na mikakati iliyojiwekea VETA na  serikali  kwa ujumla katika kutanua wigo ili kutoa wa elimu ya Ufundi stadi hata kwa jamii ambayo bado haifikiwa na miundombinu ya vyuo vya VETA mahali walipo ili  nao kuwawezesha kushiriki maendeleo ya jamii.
“Hadi sasa tunao zaidi ya vijana takribani 54 waliohiti masomo yao kupitia VSOMO na kukabithiwa vyeti vyao. “nawapongeza kwa dhati vijana hawa kwa kuhitimu masomo yao leo. Pia tunao wanafunzi 25  wanasubiri kupangiwa masomo ya Vitendo ili  kuhitimu na kupata vyeti . Nitoe wito kwao kujiandaa vyema kuingia kwenye mafunzo ya viyendo laikini pia kwa watanzania hususani vijana kutumia fursa hii kujisomea masomo ya ufundi  kwa kupitia mfumo huu wa VSOMO wakiwa popote VETA itawahudumua” alisema Bukko   
 Akitangaza majina ya wanafunzi hao waliohitimu mafunzo hayo Mkuu wa chuo VETA Kipawa, Eng Lucian Luteganya VSOMO nae alibainisha kuwa, mfumo wa kusoma mafunzo ya ufundi kupitia mtandao umekuwa na tija kubwa na kuongeza wigo kwa VETA kupokea maombi ya kutengeneza kozi maalum kulingana na uhitaji wa wanaotaka kusoma kwa manufaa ya jamii zao.  Tunachofanya leo ni udhihirisho thabiti kuwa inawezekana kutumia mifumo mibadala katika kutoa elimu na kufikia malengo tuliyojiwekea, tusiwe wangumu kwenda na mabadiliko yanayoletwa na technologia kwani kwa kufanya hivyo tutazuia fursa ya kufanya shughuli zetu kwa ufanisi.  
Napenda kuwataja wahitimu wanaomaliza leo  na kutunukiwa vyeti vya VETA ni Hamadan Salum, Elvis Mahenge Simon, Mohamed Ibrahim Mohamed, Sunday Jabil, Avitus Paul, Ridhuwani Hamidu Muhimu, Eliud Mwaikamila na Deogratius
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel kupitia mradi wetu wa kusaidia jamii wa Airtel FURSA Tunajisikia fahari kuona tunaleta mabadiliko katika jamii kwa kupitia technoligia ya mtandao wa simu.  Lengo letu ni kuiwezesha jamii kujiinua kiuchumi na kuzifikia fursa mbalimbali zinazohitaji wao kuwa na ueledi wa kutosha. Tunaamini VSOMO italeta mabadiliko katika sekta ya elimu na kuchochea ongezeko na nguvukazi yenye uledi ili kukudhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri 
Tunaahidi kuendelea kushirikia na VETA na taasisi mbalimbali katika kuhakikisha tunatumia techologia ya mawasiliano katika kutatua changamoto zao mbalimbali na kuchangia katika kuboresha maisha ya jamii zinazotuzunguka na uchumi wan chi kwa ujumla.

 Mfumo wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO toka kuzinduliwa umekuwa na mafanikio makubwa ambapo hadi sasa takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 33,000 tayari wamepakua application ya VSOMO kupitia simu zao za Androad BURE, na wengine 9500 wamejiandikisha ili kujisoma  kozi mbalimbali zikiwemo za Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

No comments:

Post a Comment