Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda amewatahadharisha Viongozi wa dini nchini kujihadhari na kuwaozesha wasichana ambao hawajamaliza elimu ya kidato cha nne ili kuwakamata wazazi wote wanaoshiriki kuwaozesha watoto wao kwasababu ya kupewa mimba wakiwa masomoni.
Amesema kuwa watoto wa kike wanashindwa kumaliza masomo kwasababu ya mimba ama kuozeshwa jambo ambalo limeendelea kuisumbua serikali katika juhudi zake za kuokoa maisha ya watoto wa kike ili waendelee na masomo na kuongeza kuwa Wilaya ya Nkasi kuna tatizo sugu la mimba kwa kuwa na mimba 152 kati ya 325 kwa Mkoa mzima.
Amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini sana maisha ya watoto wa kike na inaendelea kuweka mikakati ya kila namna ili kuhakikisha kuwa wasichana hao wanapata elimu stahiki, kwa kuanza na elimu bure na kuendelea na mikakati ya marekebisho ya sheria kadhaa ili watoto wa kike waendelee na masomo.
“Haiwezekani mtu anatakatisha fedha hapati dhamana, halafu mtu anampa mimba mwanafunzi na kisha anapata dhamana, tunakoelekea ili uolewe lazima uwe na “leaving Certificate” ama tujue kuwa hukusoma kabisa ili tuwahoji wazazi, mwananfunzi ambae ataolewa kwa kukatishwa masomo kamata wote na funga miaka 30, wazazi wa pande mbili, aliyeoa, aliyeolewa, wanaoshangilia, aliyefungisha ndoa wote miaka 30 jela,” alifafanua.
Aidha, amewashauri wanaharakati kuungana pamoja katika kuwaelimisha watoto wa kike na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha mimba zinapungua na kuwa vitendo hivyo haviendelei, ili kuwainua watoto wa kike kielimu.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya katika majumuisho ya ziara yake ya siku moja katika Mkoa wa Rukwa kwa kutembeleavituo vya afya, Shule zinazoendelea kujengwa pamoja na miradi ya maji.
Sambamba na hilo Mh. Kakunda pia ameagiza kutosajili vijiji, vitongoji wala kupeleka umeme kwenye hifadhi na kuwaondoa wale wote waliopo kwenye hifadhi na kusisitiza kuwa wananchi wasidanganyike na viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwambia kuwa watawalindwa ili kuendelea kuharibu hifadhi, jambo hilo halipo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Milundikwa Pius Msongoli wakati alipotembelea shule hiyo inayoendelea kujengwa huku serikali ikichangia shilingi milioni 250 za ujenzi wa shule hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (Kaunda suti Nyeusi) akitoa maagizo ya kuwaondoa wale wote waliopo ndani ya hifadhi ya msitu wa mfili, kwa kuwa wanachangia kuharibu chanzo cha maji na bwawa la Mfili.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya ujenzi wa maabara inayoendelea kujengwa katika shule ya sekondari Milundikwa mbele ya Mkuu wa Shule hiyo Pius Msongole, Katibu tawala wa Wilaya ya Nkasi Festo Chonya pamoja na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Emanuel Mtika.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (aliyeshika chepe) akisaidia ujenzi wa wodi za kituo cha afya Nkomolo, Wilayani Nkasi.
No comments:
Post a Comment