Saturday, November 4, 2017

TADB YATINGA HONG KONG KUTAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI KWENYE MITAJI NA MIRADI MIKUBWA YA KILIMO NCHINI KUPITIA "ONE BELT ONE ROAD"

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania hivi karibuni ilipiga hodi mjini Hong Kong kujadiliana na Taasisi mbali mbali za Hong Kong na China kuhusiana na fursa za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mitaji na uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwana Francis  Assenga walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa makampuni na taasisi kadhaa zikiwamo  Benki ya China; China Capital Fund Management (Hong Kong);  First Shanghai Capital Ltd; Mwakilishi wa China Africa Industrial Forum Ndugu Wenbao Tan ambaye ni Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha China.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation Bwana Takashi Kawasaki na Mkurugenzi wa China Biodiversity Conservation and Green Development Foundation Prof. Frederick Charles Dubee.

Miongoni mwa yaliyojiri katika mazungumzo hayo ni jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na fursa zilizopo kwenye Mikakati ya 'Silk Road Economic Belt and the 21st-century Maritime Silk Road', ujulikanao kama 'One Belt and One Road Initiative' (OBOR) ambapo kwa mujibu wa Mkakati huo, Tanzania ndio lango kuu la kuingilia Afrika kwa fursa hizo za kiuchumi na kibiashara toka Asia ambapo Tanzania inakuwa kama kiungo muhimu hivyo kuweza kunufaika zaidi ya nchi nyingine.

Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na kukuza uwekezaji kwenye miundombinu ya aina zote, viwanda vikubwa na vya kati, biashara kati ya Afrika na Asia, na Huduma mbalimbali.

Aidha, Bwana Assenga alikutana pia na akina mama wa shirika lisilo la kiserikali la kukuza uchumi kwa akina mama wa Hong Kong wanamiliki pia Shule ya Sekondari kama mchango wao kwenye huduma za jamii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bwana Francis Assenga nara baada ya kupitia Mchoro wa Ramani ya Mkakati wa Kiuchumi wa 'One Belt One Road' mjini Hong Kong hivi karibuni kwenye tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo kupitia Mkakati huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzainia (TADB) Bwana Francis Assenga (Katikati) akiwa na viongozi mbali mbali mara baada ya kumalizika kwa Kikao chake na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa China Capital Fund Management (Hong Kong) Bwana James Wang (kushoto kwake). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa First Shanghai Capital Ltd Bwana Allen Wang; Mkurugenzi wa Landmark Investments Hong Kong na Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Bunge la China Dr. Annie Wu Chung; Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama; na Mkurugenzi Mtendaji wa First Shanghai Capital Ltd Bi. Fanny Lee.
Kikao kati ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya kutafuta mitaji na uwekezaji ya Hong Kong iitwayo China Alpha Fund Management (HK) kilichofanyika katika Jengo la Two Exchange Square mjini Hong Kong hivi karibuni ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utafutaji Mitaji na Uwekezaji ya Hong Kong Bwana James Wang (Katikati). TADB iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bwana Francis Assenga (Mwenye Shati la Bluu na Tai) na kushoto kwake ni Bwana Joseph Kahama ambaye ni Katibu Mkuu wa China-Tanzania Friendship Promotion Association. Kushoto wa Kwanza ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wawekezaji wa China Alpha Fund Management (HK) Ltd Bi. Kandice Au.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bwana Francis Assenga mwenye tai nyekundu kulia kabisa akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Benki ya China Hong Kong baada ya kumalizika kwa Kikao chao mnamo tarehe 20 Oktoba 2017. Kulia kwa Bwana Assenga ni Meneja Mkuu wa BOC Hong Kong Bwana Chan Man Stephen; Katibu Mkuu wa Taasisi ya Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama; na Watendaji wa Benki hiyo Bi. Yiu Oi Yin Doris, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Biashara inayoshughulikia Taasisi za Fedha; na Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji wa Mahusiano na Mabenki, Bwana Wong Chee Him Steve, wakiwa Makao Makuu ya Benki ya China mjini Hong Kong.
Bwana Francis Assenga katikati mwenye suti ya khaki ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB akipanda miti katika Shule ya Sekondari ya China Foundation mjini Hong Kong kuashiria kuunga mkono Mapinduzi ya Mkanda wa Kijani (Green Belt Revolution) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 35 ya shule hiyo ambapo Bwana Assenga alialikwa kama Mgeni Maalum wa Shule hiyo. Wageni wengine Maalum waliotoka nchi mbali mbali ni pamoja na Bwana Joseph Kahama ambaye aliyealikwa kama sehemu ya Jopo la Washauri wa Shule hiyo kwa miaka takriban 8 sasa na Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation Bwana Takashi Kawasaki (Mwenye Suti bila Tai Kulia kabisa) toka Tokyo, Japan na Mkurugenzi wa China Mfuko wa Uhifadhi Mazingira na Maendeleo ya Mkanda wa Kijani Profesa Frederick Charles Dubee (Mwenye Mvi na Tai katikati) toka Hienola, Finland.
Kaimu Mkurigenzi Mtendaji wa TADB Bwana Francis Assenga (Kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya China Foundation Secondary School (CFSS) Bwana Au Kwong Wing, zawadi toka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati Bwana Assenga alipokaribishwa kama Mgeni Maalum wa Shule kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Sekondari hiyo Mjini Hong Kong hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliwahimiza wanafunzi wa shule hiyo kuhifafhi mazingira na kujikita kwenye teknolojia mbali mbali za kilimo cha kisasa.
Baadhi ya Wageni Maalum toka nchi mbali mbali duniani walioalikwa kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya China Foundation Secondary School (CFSS) yaliyofanyika shuleni hapo njini Hong Kong hivi karibuni. Wa Nne toka kushoto mwenye tai nyekundu ni Bwana Francis Assenga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Wawakilishi wa Tanzania Bwana Francis Assenga (Kaimu Mkuruvenzi Mtendaji wa TADB) wa pili toka kushoto na Bwana Joseph Kahama (Katibu Mkuu wa Taasisi ya China-Tanzania Friendship Association) wakikabidhiwa Zawadi ya Utambuzi wa mchango wao kwenye shughuli za kiuchumi, kilimo na huduma za jamii kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya Jiji Hong Kong. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bwana Au Kwong Wing na Kukia kabisa ni Mratibu wa Maadhimisho hayo (Mwene shati jeupe).

No comments:

Post a Comment