Thursday, November 30, 2017

SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI YAFANIKIWA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO KIELEKTRONIKI

Tangu kuzinduliwa Dirisha la Ukusanyaji Kodi kidigitali June mosi 2017 (Electronic Revenue Collection System - eRCS) ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mohamad Shein,  mawaziri kadhaa wa serikali za Muungano na serikali ya Mapinduzi; Kwa mara ya kwanza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipatia bila bugudha Ushuru mkubwa wa bidhaa na kodi ya Ongezeko la Thamani zitokanazo na makampuni ya simu.
Mfumo huu uliosukwa na vijana wa Kitanzania wazalendo, umefanikisha kuongeza mapato litokanalo na mtandao (Ciber Space) kwa Zanzibar kwa 51% kwa robo ya tatu ya mwaka 2017 ukilinganisha na miezi kama hiyo 2016. Uchunguzi uliofanyika katika robo hiyo (tatu) ya mwaka 2017 (Julai,August na Septemba 2017), umebaini Zanzibar imelipwa kupitia mfumo wa eRCS Tsh Bil 7.2 ambayo imeongezeka kwa 51% ukilinganisha na miezi kama hiyo mwaka 2016 ambapo makusanyo ya jumla ya kodi yalikuwa  Tsh Bil 3.5 pekee.
Kwa mujibu wa vielelezo vya makusanyo wa TRA, miezi mitatu kabla ya mfumo huu kuzinduliwa rasmi (April,May na June); Makampuni ya simu yalilipa jumla ya kodi ya  Tsh Bil 101.7 lakini baada ya kuzinduliwa rasimi kwa mfumo huu wa eRCS na makampuni ya simu (TTCL, HALOTEL, AIRTEL, VODACOM, ZANTEL, SMART na TIGO) kuugwa ndani ya mfumo; Kwa kipindi cha miezi mitatu pekee ( Julai,Agost na Septemba 2017), yameweza kulipa kwa njia ya kielektroniki Tsh Bil 128.9 kukiwa na ongezeko la Sh Bil 27.2 sawa na 21% huku ongezeko la kodi ya thamani ikipanda kwa 9% yaani Tsh. Bil 4.7 sambamba na ongezeko la Ushuru wa Bidhaa 29% yaani Tsh. Bil 22.
Taarifa za kiuchunguzi zimebaini serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu wowote utakao ama uliojitokeza kabla na baada ya mfumo hasa taarifa za makampuni ya simu katika matumizi yaoya kila mwezi.
Mpaka sasa, benk kadhaa nchini zimekamilisha taratibu za kuungwa katika mfumo huu na kuanza kulipa kodi kielectroniki.  Huu ni ushindi mkubwa kwa mkakati wa Rais Magufuli katika kupata njia bora za kukusanya mapato nchini. 
Ikumbukwe wajenzi wa mfumo huu ni vijana wazalendo walioaminiwa na serikali ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika katika ujenzi wa mfumo huo kutumia wataalamu na makampuni ya kigeni.
Hivi ndivyo mapato yanavyoonekana katika Dashibodi ambazo viongozi wakuu wa nchi wanaona mapato yanavyokusanywa kielectroniki kwa kutumia mfumo  wa eRCS kila sekunde.
Jedwali hili linaonyesha  Mabenk yaanza kulipa baada ya yale yaliyokamisha kujiunga na ERCS ambyo ni BANK M na AMANA BANK Tanzania ina Mabenk zaidi  ya 20

No comments:

Post a Comment