Wednesday, November 29, 2017

MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI

Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Weruweru Swalehe Msenges.kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Mnadani  Nassib Mdeme ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi .kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni .kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mnadani ,Nasib Mdeme,Diwani wa kata ya Weruweru ,Swaleh Msenges na Diwani wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi ,Wengine katika picha ni kulia mwa msimamizi wa uchaguzi ni Msimaizi Msaidizi na Mkuu wa Idara ya Fedha Juma Massatu na kushoto ni Afisa Uchaguzi wilaya ya Hai,Edward Ntakiliho.
Madiwani waliochaguliwa hivi karibuni wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Hai wakiwa na ndugu zao.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro , Ndugu Yohana Sintoo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika kata tatu zilizokuwa hazina uwakilishi limekamilika salama na kuwapata viongozi watakaowawakilisha wananchi kwenye kata husika.

Ndg Sintoo ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani wateule watatu walioshinda  kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu.

“Ndugu zangu mtakumbuka kuwa mwishoni mwa wiki kulikuwa na uchaguzi kwenye jimbo letu ambapo wananchi wa kata tatu walikuwa katika zoezi la upigaji kura kwa lengo la kuwapata viongozi wa ngazi ya udiwani baada ya madiwani wa kata husika kujiuzulu”

“Wananchi wa kata za Mnadani , Weruweru na Machame Magharibi walipiga kura ili kuwapata wawakilishi wao  ambapo zoezi hilo limekamilika bila uvunjifu wa amani kuanzia kipindi cha mikutano ya  kampeni hadi siku ya zoezi la upigaji kura na leo tunawapatia washindi vyeti vyao”

Amesema, katika uchaguzi huo jumla ya vyama vitano vilishiriki kwa kusimamisha wagombea wao kuomba ridhaa kwa wananchi ambavyo vilikuwa ni CCM, CHADEMA, ACT- Wazalendo, CUF na NCCR Mageuzi.

Vyeti hivyo vilikabidhiwa kwa Salehe Msengesi (CCM) ambaye alishinda nafasi ya udiwani katika kata ya Weruweru, Martini Munis (CCM) wa kata ya Machame Magharibi na Nasibu Mndeme (CCM) kata ya Mnadani.

Naye diwani mteule wa kata ya Weruweru, Salehe Msingesi  alisema  ahadi alizozitoa kwenye mikutano yake ya kampeni atahakikisha kuwa zinatekelezwa kwa uhakika ikiwemo kutatuankero ya barabara ambazo kwenye hiyo kata hazipitiki msimu mzima wa mwaka kutokana na uharibifu wake.

Kwa upande wake diwani mteule wa kata ya Mnadani Nasibu Mndeme
Akizungumzia utekelezaji wa ahadi alizotoa  diwani mteule wa kata ya Machame Magharibi , Martini Munisi alisema ahadi alizotoa atasimamia ili ziweze kufanikiwa kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri pamoja na Chama chake ili kuweza kusogeza huduma kwa jamii kwa wakati.



“Natambua kuwa katika kata niliyochaguliwa kuna changamoto nyingi sana ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara  , shule zote za msingi  zilizoko kwenye kata zinahitaji ukarabati wa majengo haswa shule ya Msingi Kyeri ambayo jiko lake limeanguka na linahitaji ukarabati wa haraka  ”alisema.

No comments:

Post a Comment