Monday, November 27, 2017

BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akikabidhi moja ya kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania.

Baadhi wa watoto wanufaika na kadi za bima wakiwa na walezi wao wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu


Baadhi ya wafanyakazi wa Kitengo cha magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao ni mayatima
Baadhi ya wafanyakazi BancABC Tanzania wakifuatilia kwa umakini hotuba  ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao ni mayatima.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kitego cha wateja wakubwa na wadogo wa BancABC Joyce Malai wakati wa kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania.

Picha ya Pamoja
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu aikisisita jambo kwa Mkurugenzi wa Kitego cha wateja wakubwa na wadogo wa BancABC Joyce Malai wakati wa kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania. 

BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imeshirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kutoa huduma ya bima ya afya itakayofaidisha watoto 100 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia mradi mpya wa afya wa Muhimbili uliozinduliwa leo.

Akizindua mpango huo wa Afya wa Muhimbili Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliishukuru BancABC kwa kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili katika suala hilo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa watoto.

Alisema mradi huo wa Muhimbili kushirikiana na BancABC unaendea sambamba kabisa na malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma ya Afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani watoto ndio moja ya makundi ambayo huathirika sana wasipopatiwa huduma za Afya za uhakika.

“Natoa wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa na BancABC kwa ushirikiano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafungulia watoto wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha tasilimu pale mtoto anapougua,” alisema.

Alitoa wito pia kwa watoa huduma za kifedha nchini pamoja na mashirika mengine kuhakikisha yanaiga mfano huo wa BancABC kwani wizara yake iko tayarikushirikiana na taasisi ambazo ziko tayari kuimaisha huduma katika sekta ya afya hasa upande wa utoaji huduma.

Naye Mkuu wa Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati, Bi Joyce Malai alisema BancABC inatambua umuhimu wa kuwa kampuni inayowajibika katika masuala ya kijamii kwa kurudisha kwa jamii sehemu ya faida na hasa katika sekta muhimu sana ya afya, dhamira hii ya BancABC kusaidia kwenye kuwezesha Afya ya watoto ni yamsingi sana kwa kuwa pia inasaidia serikali kufikia malengo yake.

Alisema baada ya kufungua akaunti hizo, wazazi wa watoto wenye akaunti hizo watakuwa wanahimizwa wakewe hela mara kwa mara kwa ajili ya bima ya watoto wao ili wapate huduma kupitia akaunti hizo za Mwangaza Junio Kids Accountambayo haina tozo ya kila mwezi.

Bi Joyce Malai aliongeza kuwa huduma hiyo ya bima haitakuwa na masharti kuhusu umri. “Wazazi wanaweza kufungua akaunti kwa mtoto zaidi ya moja na kuweka fedha kiasi chochote wanachotaka kwani itasaidia kuhakikisha watoto wao wana bima,”. 

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa, Prof. Lawrence Museru, aliishukuru BancABC kwa ushirikiano huo na kusema hatua hii haitasaidia watoto kupata tu huduma za afya kwa kupitia bima, bali itawajengea pia utamaduni wa kuweka akiba katika benki kuanzia utotoni hadi wanapokuwa watu wazima ili wapange mambo yao vizuri .

“Kwa sasa akaunti hizi zitafunguliwa na wazazi wao ila watakuwa wakitambua umuhimu wa huduma hii na wataendelea nayo hadi ukubwani,"alisema na kutoa rai kwa wazazi watumie fursa hiyo vizuri.

No comments:

Post a Comment