Sunday, October 29, 2017

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO AWATAHADHARISHA WAFUGAJI KUACHA KUWADHURU WANANCHI WANAOTOA TAARIFA ZINAZOSAIDIA SERIKALI



Naibu waziri wa Mifugo  na Uvuvi, Abdallah  Ulega  amewatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru  wananchi waliotoa taarifa  zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.
Naibu waziri huyo ametoa tahadhari hiyo leo wakati akizungumza  na wakazi wa kata za Mgagao na  Kirya  zilizopo wilaya  Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Amesema Serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama  vipo makini na kuhakikisha  usalama wananchi wa eneo.
Amesema Serikali  ipo makini  na ina macho na masikio  ya kutosha na ipo kila mahali na kwamba kama kuna mpango mbaya dhidi ya wananchi waliotoa taarifa hizo hautafanikiwa.
"Jambo  limeshapita acheni kutafuta mchawi. Mkae mkijua  kwamba Serikali  ina mkono mrefu atakayethubutu  kutenda mambo ataishia kwenye vyombo vya dola," amesema Ulega.
Ulega amedai kupata taarifa  za kuwapo kwa baadhi ya wafugaji kuanza vikao  vya kumtafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo
Mbali na hilo, naibu waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali  ya Rais John  Magufuli  ipo makini na imelenga kuwatetea wanyonge  na kwamba, haina nia ya kuchukua mifugo ya wafugaji  kwenye mchakato wa upigaji wa chapa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega  akizungumza na wanachi wa  kata za Mgagao na  Kirya  juu ya kuwatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru  wananchi waliotoa taarifa  zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.
 Mmoja wa wananchi akitoa kero yake mbele ya  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega wilaya  Mwanga mkoani Kilimanjaro.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega akiwasili katika  kata Mgagao na  Kirya  wilaya  Mwanga  ikiwa ni sehemu ya  ziara yake ya kikazi mkoa wa  Kilimanjaro.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya  Mwanga wakiangalia zizi la ng’ombe lilokuwa likihifadhi mifugo iliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni na kukamatwa na Serikali.

Semu ya wananchi wakimsikiza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega leo  mkoa wa  Kilimanjaro.Picha na Emmanule  Massaka,Glob ,jamii Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment