Saturday, October 28, 2017

NAIBU WAZIRI NISHATI AFANYA ZIARA KATIKA KITUO CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME KILICHOPO ZUZU DODOMA

Na Veronica Simba - Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo eneo la Zuzu mjini Dodoma, leo Oktoba 28, 2017.

Akiwa amefuatana na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, Naibu Waziri Mgalu, ametembelea Kituo hicho ili kujionea utendaji kazi wake.

Akitoa malelezo kwa Naibu Waziri, Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina amesema kuwa, Kituo hupokea msongo wa umeme wa kilivolti 220 katika njia tatu ambazo ni Mtera, Iringa One na Iringa Two. Aidha, ameongeza kuwa, Kituo kina transfoma mbili za kupoza umeme ambapo kila moja ina uwezo wa kutoa megawati 24 za umeme hivyo kufanya jumla yake kuwa megawati 48.

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme kwa Mkoa wa Dodoma, Meneja Temu ameeleza kuwa kwa sasa huduma ya nishati hiyo muhimu imerejea katika maeneo yote baada ya jitihada za Shirika hilo katika kutatua matatizo yaliyojitokeza hivi karibuni.

Akihitimisha ziara yake katika Kituo hicho, Naibu Waziri Mgalu amewasisitiza viongozi wa TANESCO kuhakikisha huduma ya umeme wa uhakika inaendelea kutolewa kwa wateja katika maeneo yote.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia) kuhusu utendaji kazi wa Kituo hicho. Wengine pichani (kutoka kushoto) ni Msaidizi wa Naibu Waziri, Ngereja Mgejwa, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akiangalia kwa makini, kupitia Kompyuta, namna umeme unavyopokelewa katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu, Dodoma na kusambazwa kwa wateja. Anayetoa maelezo (kulia) ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina. Katikati ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akimwonesha Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), namna umeme unavyopokelewa kituoni hapo na kusambazwa kwa wateja.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia). Wengine pichani ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (wa pili kutoka kulia), Msaidizi wa Naibu Waziri, Ngereja Mgejwa (wa pili kutoka kushoto) na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (wa pili kutoka kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), wakati Naibu Waziri alipotembelea Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Wengine pichani ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Bosco Mgina (kulia) na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), wakati Naibu Waziri alipotembelea Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Kulia ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akiwa katika ziara ya kukagua Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma. Kulia ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia), alipotembelea Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Kushoto ni Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akikagua Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina.

No comments:

Post a Comment