Na Beatrice Lyimo- MAELEZO,DODOMA.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa
kuzindua mfumo wa kielektoniki wa kuandaa Mipango , Bajeti na Ripoti kwa
Mamlaka ya Serikali za Mitaa(PlanRep) na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji wa
Taarifa za Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS).
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Mkurugenzi msaidizi
anayeshughulikia masuala ya TEHAMA Ofisi ya Rais – TAMISEMI Baltazar
Kibola amesema kuwa mifumo hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Septemba 5, 2017
katika ukumbi wa LAPF Mkoani Dodoma.
Akifafanua
Bw. Kibola alisema kuwa lengo la mifumo hiyo ni kusaidia kuja na mfumo
mmoja wa kitaifa utakaowezesha kuwa na utaratibu wa kuandaa mpango na
bajeti ambapo utasaidia Hamlashauri zote nchini kuwa na muundo mmoja wa
uandaaji wa mipango na Bajeti za Serikali.
Aidha
alisema kuwa lengo la Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma
(PS3) ni kushirikiana na Serikali katika kuimarisha mfumo ili kusaidia
uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika
ngazi ya kila kituo husika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka Mradi wa
uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dkt. Gemin Mtei alisema kuwa
lengo la mradi huo ni kufanya maboresho ya mifumo katika Sekta za Umma
ili kuongeza ufanisi.
“Mradi
huu unalenga kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la
Utawala Bora, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha na pia katika maeneo ya
TEHAMA ambapo utasaidia ni namna gani mifumo inawezeshwa kufanya kazi
kwa urahisi” amesema Dkt. Mtei.
Aidha
Dkt. Mtei amebainisha baadhi ya maeneo yaliyolengwa kufanyiwa maboresho
ikiwemo utoaji wa huduma, kutambua watoa huduma na pia kuwekeza kwa
watoa huduma ili kuwezesha wananchi kuweza kunufaika na huduma hizo.
Vile
vile Dkt. Meti alisema kuwa Mfumo wa kielektroniki (PlanRep)
iliyoboreshwa na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji wa Taarifa za Fedha kwenye
Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS) Mradi wa (PS3) ikiwa ni mradi wa miaka
mitano (2015 – 2020) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa
(USAID) kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
Naye
Mtaalamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago amesema kuwa
mfumo umeundwa kwa kuzingatia Ubora, Usimamizi wa fedha, ufanisi katika
utendaji kazi wa umma, kupunguza gharama za usimamizi na utendaji wa
kazi.
“Mfumo
uliokuwa ukitumika awali ulitumia gharama nyingi, muda mwingi na pia
ulihusisha watu wengi kukaa kusafiri kukaa pamoja sehemu moja, ila mfumo
huu ulioboreshwa umerahisisha utendaji kazi na kupunguza gharama
iliyokuwa ikitumika awali” amesema Rwamiago
Akibainisha
faida za mifumo hiyo kwa Serikali Rwamiago amesema kuwa itawezesha
ufuatiliaji kuanzia ngazi za vituo vya Afya, Zahanati na shule hivyo
utawezesha upatikanaji wa taarifa kutoka katika kila kituo kwa wakati.
Vilevile
amesema kuwa mifumo hiyo ina manufaa katika ngazi zote za utendaji
hivyo itasidia uunganishaji wa Taarifa kuhusu fedha za Serikali kutoka
katika ngazi ya vituo hadi Halmashauri mpaka ngazi ya Taifa.
“Mifumo
hiyo imeandaliwa katika ubora kwa kuzingatia changamoto zilizokuwepo
awali kwa lengo la kuleta ufanisi katika utekelezaji wa kazi za
Serikali” alifafanua Rwamiago.
Mradi
wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni mradi uliounganisha
Mikoa yote ya Tanzania na Halmashauri zake ambapo wataalamu wa masuala
ya Mipango, Bajeti,Waganga wakuu wa Wilaya, Makatibu Afya, Mweka Hazina
kutoka katika kila Halmashauri wamepatiwa mafunzo kuhusu Mifumo hiyo.
Mkurugenzi
Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI
Bw. Baltazar Kibola akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma
kuhusu uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na
kutoa Ripoti za Malaka ya Serikali za Mitaa utakaozinduliwa na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Septemba
5,2017 mjini Dodoma kulia ni Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka
mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei na kushoto ni Mtaalamu kutoka ofisi ya
Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago.
Mkuu
wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei
akizungumzia faida za mfumo huo wakati wa mkutano na vyombo vya habari
leo mjini Dodoma. Kushoto ni.Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia
masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola.
Mmoja
wa Wataalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akiongea
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo mjini Dodoma. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya
Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola.(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo ,Dodoma
No comments:
Post a Comment