Thursday, September 7, 2017

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATIA SAINI MKATABA WA UWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA MACHINJIO NA USINDIKAJI NYAMA CHA NGURU MKOANI MOROGORO

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa Uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji wa Nyama cha Nguru 'Nguru Hill Ranch Ltd' kilichopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S.Badrinath na katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari.
 Baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo.
 Wadau wakifuatilia hafla hiyo.

Wadau.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S.Badrinath, akitoa hotuba yake katika hafla hiyo.
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Regina Chonjo, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini wa makubaliano ya Uwekezaji katika Machinjio ya Kisasa ya Nguru mkoani Morogoro.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla hiyo.
 Sehemu ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari, akitoa hotuba yake kabla ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga, kusaini makubaliano ya uwekezaji katika machinjio ya kisasa ya Nguru Wilayani Mvomero.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akisaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama cha Nguru Wilayani Mvomero.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S. Badrinath, baada ya kusaini makubaliano ya uwekezaji katika machinjio ya kisasa ya Nguru.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama.

Eneo litakalotumika kupitishia ng'ombe wakati wakienda katika machinjio hayo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji katika machinjio ya Nguru.
Picha ya pamoja.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Eneo la machinjio ya kisasa ya Nguru.
Eneo la Ranch ya Nguru.
Maeneo ya machinjio ya Nguru.

NA MWANDISHI WETU, Mvomero-Morogoro

MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanya uwekezaji wa Dola za kimarekani  Milioni 3.90 katika kiwanda cha machinjio  na usindikaji nyama cha Nguru ‘Nguru Hills Ranch Limited’ kilichoko nje kidogo ya Morogoro Wilaya ya Mvomero.

Akizunguza katika  uwekaji wa saini kwenye mkataba wa uwekezaji, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga, alisema uwekaji wa saini umefikiwa baada ya tathini ya kina iliyofanywa na mfuko huo.Alisema mfuko umejiridhisha  kuhusu usalama wa rasilimali za wanachama kwenye uwekezaji huo.

“Tunatambua kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika viwanda lakini LAPF imeona fursa hii ni moja wapo ambayo inakidhi vigezo vyote vya ajenda ya uwekezaji”alisema Sanga.

Alisema LAPF imewekeza kwenye kiwanda hicho kwa ubia na kampuni ya ‘Eclipse Investments LLC’ inayotokana na kampuni tanzu ya Zubair Corporation ya Oman na kampuni ya ‘Busara Investments LLP’ na kufanya wabia kuwa watatu.

“Kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na LAPF ni USD 3.9 Milion ambayo ni sawa na asilimia 39 ya hisa za kampuni,ambapo Eclipse Investments LLC inaa hisa asilimia 46 na Busara Investments LLP ina hisa asilimia 15”alisema  Sanga.

Alisema kiwanda hicho kina ukubwa wa ekari 6,000 ambapo ekari 1,200 zimejengwa miundombinu ya malisho ya mifugo kwa kipindi kisichopungua siku 90 kwaajili ya kuwanenepesha na kuwapa ubora kabla ya kuchinjwa.

Sanga alisema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo kuchinja na kuchakata ng’ombe 300 na mbuzi 2,000 kwa siku na kusafirishwa mara moja.

“Nyama itakayozalishwa kwa kiwango kikubwa itasafirishwa nje kwenye nchi za mashariki ya kati na mashariki ya mbali ambako soko ni kubwa na Oman”alisema Sanga.

Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 500 na nyingine zisizo za moja kwa moja na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya viwanda vingine.

No comments:

Post a Comment