Wednesday, September 27, 2017

JAFO AAGIZA MAAMUZI YA HARAKA YA UPANUZI WA HOSPITALI YA TUMBI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua upanuzi wa Hospitali ya Tumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maagizo kwa uongozi wa mkoa wa Pwani na watendaji wakuu wa Shirika la Elimu Kibaha ambao Hospitali ya Tumbi ipo chini yao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ramani ya upanuzi wa jengo la hospitali ya Tumbi Kibaha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akimsalimiana na mgonjwa ambaye ni mlemavu wa viungo katika Hospitali ya Tumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliyopo mkoani Pwani.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi ameutaka Uongozi wa Shirika la Elimu Kibaha na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kukaa pamoja na kufanya Maamuzi ya haraka ndani ya wiki moja wafikie makubaliano ya uendelezaji wa ujenzi wa jengo jipya la upanuzi wa hospital ya Tumbi ambayo ni hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani.

Jafo ameoneshwa kukerwa na ugoigoi wa kufanya maamuzi unaoendelea licha ya serikali kupeleka fedha kiasi cha sh.milioni 685 katika mwaka wa fedha 2016/2017 lakini mpaka sasa wameshindwa kufanya Maamuzi.

Naibu Waziri Jafo amesema kitendo hicho kinachelewesha kuwapatia huduma bora wananchi.Kutokana na hali hiyo, Jafo amewaonya watendaji hao na kuagiza hadi wiki ijayo wawe wamekamilisha mkataba wa makubaliano na ujenzi uanze mara moja.

Upanuzi wa hospitali ya Tumbi unalenga kuimarisha miundombinu ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi mbalimbali wa mkoa wa pwani na mikoa mingine hapa nchini kwani kwa muda mrefu hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kwa siku ikihusisha pia majeruhi wengi wanao pata ajali katika barabara ya Morogoro.

No comments:

Post a Comment