Tuesday, August 1, 2017

WAUZA DAWA FEKI ZA KUUWA WADUDU WA ZAO LA PAMBA KUKIONA –MPINA



NA EVELYN MKOKOI – MWABUSALU MEATU

Hatua kali zitachuliwa kwa wafanyabiashara wanaouza dawa feki za kuuwa wadudu wa zao la Pamba nchini, Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa akizungmza na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba katika kata ya Mwabusalu Wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake jimboni Kisesa.

Mpina alisema kuwa wapo wafayabiashara wanaodhoofisha wakulima wa zao la Pamba kwa kuwauzia madawa yasiyo na nguvu na kutoweza kufanya kazi kabisa katika zao la Pamba na kupelekea kufa kwa zao hilo na kuwataka watu hao kuwaletea wakulima dawa bora kabisa na kinyume na hapo wizara husika itachukua hatua dhidi yao.

Aidha amewataka wakulima wa kijiji hicho kinacholima zao hilo la mfano nakutoa mbegu Bora Pekee ya pamba nchini kuacha kilimo cha mazoea na kutumia fursa hiyo kuangalia kwanza maeneo wanayoishi kutokana na faida itokanayo na biashara ya zao la pamba kuninunulia chakula cha kutosha na kutoka kwenye nyumba za tembe na kujenga nyumba za kisasa.

Sambamba na hilo Mpina amewataka wakulima hao kuzingatia sauala la utunzaji wa mazingira kwa kuyaandaa mashamba yao kwa wakati huku wakizingatia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi wanayokabilina nayo.

Awali, Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Pamba cha Geki Investiment limited na kuutaka uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji mapema mwakani ili wakulima wa kata ya Mwabusalu waweze kunufaika kutokanana mauzo ya pamba yao karibu. “Serikali hii inalenga katika kuinua na kuimarisha uchumi wa viwanda hivyo kiwanda hiki sasa wakati umefika wakuanza uzalishaji kisikae hapa na kutumika kama ghala kianze kazi mara moja, vinginevyo hatuta mvumilia muwekezaji huyu kama atashindwa Wizara husika itafanya kazi yake”. Alisisitiza Mpina.

Serikai ya awamu ya tano toka iingie madarakani imepandisha bei ya zao la pamba kutoka bei ya awali ya shilingi 600 kwa kilo mpaka mpaka sh. 1,200 imeelezwa kuwa kata ya Mwabusalu, ni kata ambayo imepata upendeleo kwa wakulima kuuza Pamba hiyo kwa kiasi cha shilingi 1,320 kwa kilo.

Tafiti zinaonyesha kuwa kata ya Mwabusalu inalima Pamba ambayo pamoja namatumizi mengine inatoa Mbegu ambayo inapatika pia katika maeneo mawili tuu nchini yanii mwabusalu na Ingunga Mkoani Tabora.


katika Picha Roli lililobeba pamba za wakulima tayari kwenda kuuzwa
Naibu Waziri Mpina akingalia ubora wa Pamba ya wakulima katika kijiji cha Mwabusalu leo.
Naibu Waziri Mpina akipima furushi la Pamba katika Mzani Maalum kabla ya kuongea na baadhi ya wakulima wa Pamba katika kijiji cha Mwabusalu jimboni kisesa leo.
Baadhi ya wakulima wa Pamba wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (hayupo pichani) alipokuwa akingumzanao katika kijiji cha Mwabusalu mapema leo.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba kijijini Mwabusalu, Meatu Mkoani Simiyu leo.

No comments:

Post a Comment