Friday, August 25, 2017

UKAID NA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAZINDUA PROGRAM YA MAFUNZO KWA WATUMISHI

Wafanyakazi watano wa Wizara ya Fedha na Mipango (Walioketi) waliopatiwa udhamini wa masomo nchini katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAID-DFID), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa British Council-Tanzania ambao ndio waratibu wa Program hiyo ya miaka mitano, itakayogharimu Shilingi bilioni 3.6 kwa  lengo la kuongeza ujuzi na umahili wa rasilimali watu katika masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za Umma na Sheria za kimataifa. Kutoka kushoto Harieth Lubinga, John Kabiti, Susan Mbayuwayu, Peter Kalugwisha na Gloria Mduda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiongea ofisini kwake na Mkurugenzi Mkazi wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo kutoka Serikali ya Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy, kuhusu masuala mbalimbali ukiwemo ufadhili wa miaka mitano wa Taasisi hiyo wa masomo ya juu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), wakielekea katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa ufadhili wa miaka mitano wa masomo ya juu kwa watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza wenye thamani za shilingi bilioni 3.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Mkuu wa Shirika la Msaada la Uingereza (UKAID) nchini Tanzania Beth Arthy (wa pili kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) wakielekea katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo ya mafunzo ya juu kwa ngazi ya Shahada ya Uzalimili kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza kuhusu masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha umma na sheria kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango uliotolewa na Serikali ya Uingereza.
Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly, akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo ya juu katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la UKAID-DFID utakaogharimu shilingi bilioni 3.6. British Council Tanzania ni waratibu wa mpango huo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) akizungumza katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la  UKAID-DFID, uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya ufadhili wa masomo ya Juu katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango katika ngazi ya shahada ya uzamili kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza UKAID-DFID wenye thamani ya shilingi bilioni 3.6, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na viongozi waandamizi wa UKAID-DFID, British Council-Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango walionufaika na ufadhili huo (kushoto) wakifurahia baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo kwa ngazi ya shahada ya uzamili katika vyuo vikuu vya nchini Uingereza katika Nyanja za uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za umma na sheria za kimataifa uliotolewa na Serikali ya Uingereza kwa Wizara hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliopata ufadhili wa Mafunzo kutoka UKAID-DFID, muda mfupi baada ya kuzindua rasmi program hiyo, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)​

No comments:

Post a Comment