Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo
ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo ya Kilimo, Uvuvi na
Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na
Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo
ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Nanyumbu akiwasili katika banda la wizara ya Kilimo Mifugo na
Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto)
ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo kwa Mkurugenzi wa Farm Base Ltd Ndg Suleiman Msellem kuhusu Pembejeo za kilimo, na ushauri wa Kilimo, Uvuvi na
Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na
Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto)
ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo kwa Mkurugenzi wa
Farm Base Ltd Ndg Suleiman Msellem kuhusu Pembejeo za kilimo, na ushauri
wa Kilimo, Uvuvi na
Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na
Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi
Na Mathias
Canal, Lindi
Wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla
wameombwa kushiriki kwa wingi katika Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za
Nanenane yanayofanyika kwa siku 8 katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo ambaye pia ni
Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho.
Mhe
Wangabo alisema kuwa Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo hutoa
changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira
hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini hivyo
wananchi kushiriki kwao kutawahakikishia elimu mbadala ya kilimo chenye tija
kwao na Taifa kwa ujumla.
Maonesho
hayo yanabebwa na kauli mbiu mahususi kwa mwaka huu 2017 isemayo "Zalisha
kwa Tija Mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati"
ikiwa imedhamiria kwa kiasi kikubwa kumkwamua mwananchi na mkulima wa kawaida
kuondokana na uduni wa mazao wakati wa mavuno.
Katika
Maonesho hayo Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau
wote wa kilimo na mifugo wanatekeleza jukumu kubwa la kuwaelimisha wakulima na
wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi
kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.
Teknolojia/Bidhaa zinazooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za
mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo
piaTaasisi za kitafiti ambazo zitaonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza
tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi
ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya
kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi
wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa.
Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa
mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo
Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili,
Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.
Hivyo kwa wingi wao wananchi waishio Kanda ya kusini katika mikoa ya Lindi na
Mtwara wanapaswa kutumia fursa hii ambayo inatokea katika kipindi kimoja pekee
katika kila mwaka.
Mhe
Wangabo alisema kuwa Tatizo
kubwa linalokabili sekta ya kilimo na ufugaji nchini kutozingatia kanuni bora
na za kisasa za kilimo na Ufugaji. Nimefurahishwa sana kuona kwamba katika
maonyesho haya kuna Taasisi za utafiti zinazozalisha mbegu za kisasa.
Alisema kuwa zipo changamoto zinazokabili sekta ya
kilimo na mifugo nchini ikiwa ni pamoja na ukame, upungufu wa madawa ya mifugo,
uchache wa maafisa mifugo, upungufu wa majosho, uvuvi haramu na miundombinu
duni ya kusafirisha mazao ya mifugo.
Hata hivyo Serikali itaendelea kutatua changamoto hizo
kwa kuongeza maafisa ugani ili
wawawezeshe wakulima kuzingatia kanuni za kilimo na ufugaji bora; kuhamasisha
wananchi kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji, kuvuna maji ya mvua, kuchimba
malambo, kuongeza majosho, kuongeza madawa ya mifugo na kuhamasisha wakulima na
wafugaji kutumia zana bora za kilimo.
No comments:
Post a Comment