Monday, July 3, 2017

SINGIDA UNITED KUINGIA KAMBINI KESHO, YANUNUA GARI LA MAMILION KWA AJILI YA TIMU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


SINGIDA United inaingia kambini kesho kwa ajili kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Vodacom  huku ikizitahadharisha timu za Simba na Yanga kuwa hawana undugu nao na kama kuna wanaodhani hivyo wanaota ndoto za mchana kwani wataujua ukweli baada ya kuanza msimu mpya wa ligi utaoanza mwezi Agosti.


Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa klabu hiyo Festo Sanga mbele ya Waandishi wa Habari na kuondoa utata ulioanza kujitokeza kuhusu baadhi ya viongozi kuwa na mapenzi na timu hizo kongwe nchini.

Kumekuwa na dhana kuwa Singida inaweza kuwa undugu na karibu na Yanga kwakua kiongozi wake mkuu Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, kocha mkuu wa timu hiyo Mholanzi Hans Pluijm na msaidizi wake Fred Minziro wote wakiwa ni wapenzi wakubwa wa mabingwa hao wa ligi kuu msimu uliopita.

"Inawezekana kuna viongozi wana mapenzi na timu za Simba na Yanga ila Singida United haitambui hilo, na mkitaka kuamini kauli yangu subirini ligi ianze ndiyo mtaona kitakacho tokea," alisema Sanga.

Singida itaingia kambini kesho jijini Mwanza kwa ajili ya kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi mwezi ujao ambapo imepanga kutafuta mechi za kirafiki kutoka nchi za Kenya, Uganda na Rwanda.

Wakati huo huo Sanga alisema wamefanikiwa kununua basi la klabu hiyo aina ya Dragon lenye thamani ya shilingi milioni 350 watakalo litumia kusafiri sehemu mbalimbali kuanzia sasa.

" Tumefanikiwa kununua basi kwa ajili ya safari zetu za timu ndani na nje ya nchi kuanzia sasa," alisema Sanga.a

  Muonekano wa gari la Singida United linaloratajiwa kutumiwa na wachezaji wa timu hiyo katika msimu mpya wa ligi kuu.


Meneja wa klabu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kulitambulisha basi lao jipya litakalotumika kwa safari za ndani za timu ya Singida United.

No comments:

Post a Comment