Monday, July 24, 2017

NUSU FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS, MCHENGA, KURASINI ZASHIKA KASI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yamefikia katika hatua ya nusu fainali kwa timu nne kuumana mwishoni mwa wikiendi iliyopita huku Mchenga Bball Stars na Kurasini wakiibuka na ushindi.

Michezo hiyo iliyochezwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay ilikuwa ni hatua ya kwanza ya mechi za nusu fainali ambapo wikiendi ijayo itaendelea tena ikiwa ni hatua ya pili.

Baada ya kumalizika kwa hatua tatu za mechi ya nusu fanilai, mshindi wa jumla wa mechi hizo ataingia moja kwa moja katika fainali ya Sprite BBall Kings inayotarajiwa kufanyika mwezi Agost mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.

Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wikiendi iliyopita, wiki ijayo timu hizo zitaumana tena mpaka katika hatua ya tatu na timu zilizopata alama nyingi ndiyo zitafanikiwa kuingia hatua iya fainali.

"Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya leo na katika michezo ya hatua zijazo ndiyo watakaofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings,"amesema Basilisa.

Katika mechi zilizochezwa wikiendi hii mchezo wa kwanza uliwakutanisha TMT dhidi ya Kurasini ambapo Kurasini walitoka na ushindi wa vikapu 87 kwa 80, na mchezo wa pili timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers 

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio inaendelea tena wiki ijayo katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay na mshindi kamili ataondoka na kitita cha shiling milion 10.
Mchezaji wa timu ya Mchenga (jezi nyeusi) akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Flying Dribblers katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.
Mchezaji wa timu ya Flying Dribblers (jezi nyeupe) akiwa amemiliki mpira katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.

No comments:

Post a Comment