Wednesday, July 5, 2017

KAIMU JAJI MKUU, WAZIRI MWIJAGE WATEMBELEA BANDA LA WCF


 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto), akikaribishwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Sebera Fulgence, alipotembela banda hilo kwenye hema la Jakaya Kikwete viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Julai 4, 2017. Mhe Profesa Hamisi  alitumia kwa uchache dakika 15 akiwa na shauku ya kupata taarifa zaidi kuhusu kazi na majukumu ya Mfuko huo. 

Mhe Profesa Hamisi alielezwa kuwa Mfuo huo umeundwa mahsusi kwa ajili ya kutoa fidia stahiki kwa Mfanyakazi aliyepata ugojnwa au kuumia mahala pa kazi. Hali kadhalika, alielezwa kuwa pamoja na kwamba Mfuko huo  ni wa Hifadhi ya Jamii, namna ya uchangiaji wake unatofautiana na Mifuko mingine, ambapo Mwajiri ndiye anawajibika kisheria kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi wakati Mifuko mingine, wachangiaji ni wote, mwajiri na mwajiriwa. 

Wakati hyuo huo, Waziri anayehusika na sekta ya Viwanda na Biashara, sekta ambayo inatoa ajira kubwa kwa wafanyakazi, naye alipata fursa ya kutembelea banda hilo ambapo kama ilivyokuwa kwa Kaimu Jaji Mkuu naye alielezwa majukumu yanayotekelezwa na Mfuko ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Sebera Fulgence, alimueleza kuwa sekta ya viwanda na biashara ni miongoni mwa sekta zinazotoa wanachama wengi kwenye Mfuko huo, ukiachilia elimu na afya na kwamba Mfuko umekuwa ukiendelea kutoa elimu zaidi kwa waajiri kuhusu umuhimu wa kuchangia wafanyakazi wao kwa manufaa ya mwajiri na mwajiriwa pindi yanapotokea madhara. 

Mfuko wa WCF ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi (sura 263 marejeo ya mwaka 2015).
 Profesa Ibrahim Hamisi Juma, akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence.(hayupo pichani)
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia maeelzo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia maelezo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akizungumza jambo na Maafisa wa WCF, Bw. Sebera Fulgence (wapili kushoto) ambaye ni Afisa Uhusiano Mwandamizi na Bi.Bi.Inocencia William
 Mhe. Waziri Mwijage, (kulia), akiagana na Bw. Sebera baada ya kutembeela banda hilo na kuelimishwa kuhsuu majukumu ya Mfuko.
 Maafisa wa WCF wakiwa tayari kuwahudumia wananachi
 Bi.Bi.Inocencia William, (kushoto), afisa wa WCF akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye banda la Mfuko huo
 Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za shughuli na majukumu yanayotekelezwa na WCF
 
Mhe. Profesa Hamisi akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka
 Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto) akiaghana na wafanyakazi wa WCF

 Bw. Sebera akisalimiana naMchambuzi wa soka hapa nchini, Bw. Ally Mayai kwenye banda la Mfuko wa WCF


No comments:

Post a Comment