Thursday, June 15, 2017

UKATILI WA KINGONO BADO CHANGAMOTO KWA WASICHANA HAPA NCHINI

1.Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akihutubia wajumbe wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla akipata Maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi masuala ya Watoto wa Wizara yake kuhusu kazi za Wiazara wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Joheli Festo wakiangalia ripoti iliyozinduliwa leo na shirika Save the Children kuhusu hali ya ndoa za ututoni duniani wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla ,Katibu Mkuu Sihaba Nkinga na Mkurugenzi wa Shirika la Save the Children Jasminka Milavanovic wakionesha ripoti iliyozinduliwa na shirika la save the children kuhusu hali ya ndoa za utotoni duniani wakati Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla akipata Maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi masuala ya Watoto wa Wizara yake kuhusu kazi za Wizara wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.

NA ANTHONY ISHENGOMA

Wasichana Nchini Tanzania wanakumbana na changamoto mbalimbali katika makuzi yao ikiwemo ukatili wa kingono hususani mimba za utotoni kabla ya kufikia miaka 18.

Akiongea na vyombo vya habari mjini Dodoma leo katika Kongamano la maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangala amesema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 51.4 ya idadi ya watoto ni wasichana pia takwimu zinaonesha kuwa mtoto wa kike 1 kati ya 3 na wa kiume 1 kati ya 7 anakumbana na ukatili wa kingono kabla ya kufikia umri wa miaka 18.

Mhe. Kigwangala aidha amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa uwiano wa wasichana na wavulana katika elimu ya msingi na sekondari ni uwiano wa moja kwa moja (1:1), ingawa idadi ya wasichana hupungua kutokana na changamoto wanazokutana nazo ikiwa ni pamoja na mimba na ndoa za utotoni.

‘’ Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu kwa Mwaka 2012 hadi 2016 idadi ya watoto wa kike walioacha shule kutokana na kupata ujauzito ni 610 (mwaka 2011), 2,433 (mwaka 2012), 247 (mwaka 2013), 265 (mwaka 2014 na 251 (mwaka 2015). Serikali inaendelea kukabiliana na changamoto hizi ili kuhakikisha wanafunzi wa kike wanapata elimu hadi kufikia ngazi ya vyuo alisema Mhe. Kigwangala’’.

Ametaja madhumuni ya kuadhimisha siku hii kuwa ni kutoa fursa kwa wazazi, walezi na wadau wote wa haki za mtoto kutafakari changamoto zinazowakabili kama vile ukatili katika Bara letu la Afrika kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.

Maadhimisho ya siku hii hapa Nchini hutumika kutathmini changamoto zinazowakabili watoto katika upatikanaji wa haki, malezi, elimu, afya na ulinzi kwa lengo la kuboresha huduma hizi ili ziweze kumfikia kila Mtoto nchini.

Aidha amesema siku siku hii inatumika kuwakumbusha na kuwahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia jukumu lao la msingi la utoaji haki na huduma za ustawi wa Mtoto bila ubaguzi wowote. Siku hii hutumika kufanya ushawishi kwa wadau kuwekeza katika maeneo ya malezi, afya, elimu, ulinzi kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali za kumwendeleza Mtoto.

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yametokana na Azimio lililopitishwa na iliyokuwa Jumuiya ya Nchi Huru za Umoja wa Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa shule yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto, nchini Afrika ya Kusini tarehe 16 Juni 1976.

Aidha Katika tukio hilo la kusikitisha, inakadiriwa kuwa takribani watoto 700 waliuawa kikatili wakiwa kwenye harakati za kupinga mifumo ya elimu ya kibaguzi iliyokuwa inataolewa na serikali ya makaburu.

No comments:

Post a Comment