Tuesday, June 13, 2017

TAASISI ZA KIBENKI ZATAKIWA KUBORESHA MIFUMO YAO YA KIUTENDAJI

Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano (kushoto)akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Benki ya TPB,kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu TPB,Sabasaba Moshingi ,ambapo ofisi hiyo mpya ipo katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya. 
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akizindua jiwe la msingi katika benki ya TPB iliyopo eneo la Mwanjelwa. 
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindanoakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la ofisi ya benki ya TPB Mwanjelwa. 
Afisa Mtendaji Mkuu TPB SabaSaba Moshingi ,kushoto akimkabidhi ripoti ya Mwaka Msajili wa Hazina Dkt Osward Mashindano katika hafla ya uzinduzi wa ofisi mpya ya jengo la Tpb Mwanjelwa jijini Mbeya. 
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akionesha kadi maalum aliyokabidhiwa na benki ya TPB mara baada ya kuzindua jengo hilo la ofisi eneo la mwanjelwa jijini Mbeya. 
Meza kuu katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa TPB. 



TAASISI za kifedha nchini, zimetakiwa kuboresha mifumo ya utendaji kazi, ili kwenda sambamba na mabadiliko ya ukuaji wa uchumi.

Kauli hiyo, imetolewa leo na Msajili wa Hazina Dkt .Osward Mashindano, wakati akizindua Ofisi kuu ya Benki ya TPB iliyoko katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya.Amesema, wakati uchumi wa dunia unakua ni vema taasisi hizo zikajiimarisha kiutendaji ili kukidhi vigezo vya ushindani wa kibiashara ndani na nje ya nchi.

“Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta za kifedha nchini zinatoa msukumo unaotakiwa kwenye shughuli za kiuchumi, hivyo ni wakati wenu nanyi kubadili mifumo ya utendaji kazi ili kwenda sambamba na ukuaji huo wa uchumi“,alisema.

Aidha ametoa wito kwa taasisi za kifedha nchini kuhakikisha inaweka mazingira rafiki kwa wananchi wa kipato cha chini kwa kuweka gharama nafuu za huduma zao ili waweze kuzimudu.Pia, Mashindano ameipongeza benki ya TPB kutokana na na jitihada zake za kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mawakala.

Hata hivyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, alisema benki hiyo imetoa gawio kwa serikali kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 ambapo hundi hiyo inatarajiwa kukabidhiwa mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment