Wednesday, June 28, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Chama cha wananchi CUF kimeazimia kufungua kesi mahakamani dhidi ya wakala wa usajli, udhamini na ufilisi RITA kwa kukiuka sheria ya udhamini. https://youtu.be/rUN71fwnXnY

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema serikali itawachukulia  hatua wafanyakazi wa mizani za barabarani wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. https://youtu.be/ZDPhNsxsDXk

SIMU.TV: Zaidi ya wafanyakazi 300 wa kampuni ya ujenzi ya CCECC  inayojenga barabara ya Magole kwenda Turiani mkoani Morogoro wamegoma kuendelea na kazi kwa madai ya malimbikizo ya mishahara, kusainishwa mikataba bandia pamoja na manyanyaso mbalimbali. https://youtu.be/faWN633fstU

SIMU.TV: Wakazi wa mji mdogo wa Merereni wameiomba serikali kuingilia kati vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa wafanyakazi wa migodi ya wachimbaji wadogo katika eneo la Mererani. https://youtu.be/-XaY5QJ5rTo

SIMU.TV: Jeshi la kujenga taifa JKT lipo katika maandalizi ya kufufua kambi tano maeneo mbalimbali nchini ili kuwezesha vijana wengi wenye sifa kujiunga na mafunzo ya  jeshi hilo. https://youtu.be/7xZerifAMg0

SIMU.TV: Wananchi wanaofanya kazi zao mitaa ya Zanaki na Hindi jijini Dar es Salaam wamekumbwa na taharuki kubwa leo baada ya jengo moja la ghorofa kushika moto  ambapo jeshi la zimamoto lilifanikiwa kuuthibiti. https://youtu.be/UhJ5ErY5Ss4

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Temeke limewashikilia wasichana kumi na mvulana mmoja waliokutwa wakiwa wamevaa nusu uchi katika fukwe za Coco Beach na kudaiwa kujihusisha na vitendo vya ukahaba. https://youtu.be/cVt96iMqidA

SIMU.TV: Wadau wa sekta ya maziwa nchini wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili maendelo ya sekta hiyo na kufanya tathimini ya kuwaunganisha wafugaji wadogo kwa ajili ya kuchochea uzalishaji wenye tija. https://youtu.be/rUWIYFnF0Vs

SIMU.TV: Naibu waziri wa kazi vijana na ajira Antony Mavunde amewataka wananchi kutumia vyema fursa wanazopata ili kujijenga kiuchumi na kuondokana na umaskini. https://youtu.be/nZ9Ypwjk7Aw

SIMU.TV: Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imekiri kuendelea kuwashikilia rais wa shirikisho la soka TFF Jamali Malinzi na katibu wake Selestini Mwesiga kwa ajili ya mahojiano ya tuhuma za vitendo vya rushwa. https://youtu.be/V7N-zCnCqMs

SIMU.TV: Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars sasa imeelekeza nguvu zake katika mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Mauritius baada ya hapo jana kutoka ya bila kufungana na Angola. https://youtu.be/gt5W2ZaJv-s

SIMU.TV: Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kuichezea timu ya Yanga. https://youtu.be/eA6tQuTQn9M

SIMU.TV: Klabu ya Arsenal imewaahidi posho nzuri wachezaji wake nyota Alexis Sanchez na Mesut Ozil ili kuwavutia wasaini mikataba mipya. https://youtu.be/tLjHLYra6P8

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amesema amebaini kuwepo kwa askari wasio waaminifu wanaoshirikiana na wananchi kusafirisha mahindi nje ya nchi; https://youtu.be/lQxdmo1O-ng

SIMU.TV: Rais wa Tanzania Dr John Magufuli amekutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme na uchimbaji mabwawa kutoka Ethiopia ili kubadilishana uzoefu; https://youtu.be/DFCqFALY87E

SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza wapelelezi na waendesha mashitaka nchini kutenda haki na kujiepusha na vitendo vya rushwa; https://youtu.be/_RyseWgq29k

SIMU.TV: Maonyesho ya kibiashara ya 41 maarufu kama Sabasaba yameanza katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  vilivyopo wilayani Temeke mkoani Dar Es salaam; https://youtu.be/ssm6toqY38M

SIMU.TV: Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa pamoja limeridhia mikataba miwili ya kimataifa kutoka shirika la kazi duniani ILO katika sekta ya Ubaharia; https://youtu.be/mdw600-N-os

SIMU.TV: Katibu mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Shariff Hamad, amemshutumu wakala wa usajili RITA kwa kusajili bodi ya wadhamini ya chama hicho bila utaratibu;’ https://youtu.be/jEAg0R-7U8g

SIMU.TV: Tanzania imeitaka Kenya kuheshimu makubaliano ya kimkataba ya kibiashara ya Jumuiya ya Afrika mashariki baada ya nchi hiyo kuzuia kuingia gesi kutoka Tanzania; https://youtu.be/qH5C55aXEAE

SIMU.TV: Wadau wa Korosho wameazimia zao hilo kubanguliwa hapa nchini ili kuongeza thamani na kuongeza ajira kwa watanzania wenyewe; https://youtu.be/PLDOUmW5htg

SIMU.TV: Naibu wa waziri wa kilimo na ufugaji William Ole Nasha amezindua soko la biashara ya Tumbaku katika mkoani wa Kitumbaku wa Mbeya; https://youtu.be/ibG-g3baGDg

SIMU.TV: Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru inawashikilia viongozi wa TFF Jamal Malinzi na Selestine Mwesigwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha; https://youtu.be/Pw115OmHd84

SIMU.TV: Waziri wa elimu Prof Ndalichako ameagiza kila mkoa hapa nchini kutenga shule mbili kwa ajili ya kuwaendeleza wanafunzi wenye vipaji; https://youtu.be/3ruQMlNjZcw

SIMU.TV: Mshambuliaji nguli wa mabingwa wa soka Tanzania bara klabu ya Yanga Donald Ngoma amesaini kandarasi ya miaka miwili kuendelea kusalia Jangwani; https://youtu.be/GPTmzsaIq7s

SIMU.TV: Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez amekiri kuwa anatambua mchezaji wao nyota Christiano Ronaldo amekasirishwa sana na kashfa za kukwepa kodi; https://youtu.be/DWMfSdBLXgM



No comments:

Post a Comment