Na Frank Shija - MAELEZO
Wasanii nchini watakiwa kufuata taratibu na
kujiunga katika vyama vyao ili kujiweka katika mazingira rafiki ya utekelezaji
wa majukumu yao ikiwemo kusaidiana katika kutatua changamoto zinazowakabili.
Wito huo umetolewa leo na Katibu Mtendaji wa
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mungereza ambaye alimwakilisha Waziri
wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika zoezi la
kuaga mwili wa anayedaiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa, Mzee Francis Maige Kanyasu
zoezi lililofanyka Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo.
Mungereza alisema kuwa utaratibu wa kuwepo kwa
vyama vya wasanii ni wa ,uda mrefu tangu miaka ya sitini ambapo wasanii
wamekuwa wakijiunga katika vyama hivyo kwa leong la kuwa na sauti ya pamoja.
“Mhe. Waziri anasema wazee wa namna hii,na wasanii
kwa ujumla ni vizuri tukafuata taratibu kwa mujibu wa sheria, hii itasaidia
wasanii kutambulika,kujitangaza na kufahamiana,” alisema Mungereza.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura
kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga alisema kuwa Mzee Ngosha
amefariki kutokana na maradhi makubwa ya Kifua Kikuu kilichotokana na kuugua
kwa muda mrefu bila ya kupatiwa matibabu.
Aidha Dkt. Mfinanga alitumia fursa hiyo kutoa wito
kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwahi kufika katika vituo vya tiba punde
wanapohisi kuwa na matatizo ya kiafya kwani kufanya hivyo watakuwa wamejiweka
katika mazingira mazuri ya kuepuka vifo visivyotarajiwa.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malapa, Buguruni ameipongeza Serikali kwa
jitihada ilizofanya za kuhakikisha inawapata ndugu zake jambo lililopelekea
mzee Francis Kanyasu kusafirishwa na kwenda kuzikwa nyumbani kwao katika Kijiji
cha Igokero Misungwi Mkoani Mwanza.
Marehemu Mzee Francis
Maige Kanyasu maarufu Ngosha alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
mnamo tarehe 25 Mei akitokea katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kufuatia
jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto ambapo alifanyiwa vipimo na matibabu hadi mauti yalipomkuta majira ya
saa 2:30 usiku siku ya tarehe 29, Mei, 2017.Mzee Ngosha anadiawa kuwa miongoni
mwa wabunifu wa Nembo ya Taifa jambo ambalo amekufa kukiwa hakuna uhakika juu
ya suala hilo.
Picha ya Marehemu Francis Maige Kanyasu maarufu
kwa jina la Mzee Ngosha anayesaidikiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa ikiwa
katika eneo maalum la kuagia miili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati
wa zoezi la kuuaga mwili wake leo Jijini Dar es Salaam. Mwili huo umeagwa leo
na kuelekea Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi ambapo Serikali inawakilisha
na Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii – Wazee na Walemavu kutoka Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi. Beatrice Fungamo.
Mkurugenzi
wa Idara ya NGO’s kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Bw. Marcel Katemba (mwenye shati la kitenge) aliyemwakilisha Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akishiriki kubeba jeneza
lililobeba mwili wa mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) anayesadikiwa kuwa
mbunifu wa Nembo ya Taifa mara baada ya zoezi la kuuaga mwili huo kumalizika
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo. Mwili huo
umesafirishwa kuelekea Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Malapa,Buguruni Jijini Dar
es Salaam Karim Mahamoud Malapa akisaini kibali cha mazishi ya Mzee Francis
Maige Kanyasu nayesadikia kuwa mmoja wa wabunifu wa nembo ya Taifa wakati wa
hafla ya kuaga mwili wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mfanyakazi wa Hospitali hiyo Mganga Muya. Mzee Ngosha
alipokelewa katika Hospitali hiyo mnamo tarehe 25 nakufanyiwa vipimo na
kubainika na maradhi ya Kifua na kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkuta
majira ya saa 2:30 usiku wa tarehe 29 2017.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii – Wazee na
Walemavu kutoka Wizara ya Afya na maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bibi. Beatrice Fungamo akionyesha kibali cha mazishi ya Mzee Francis Maige
Kanyasu (Ngosha) anayesaidikiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa wakati wa zoezi
la kuuaga mwili huo leo Jijini Dar es Salaam. Mwili huo umesafirishwa kuelekea
Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii – Wazee na
Walemavu kutoka Wizara ya Afya na maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Bibi. Beatrice Fungamo akipokea fedha taslimu shilingi elfu hamsini na saba zilizokutwa
katika pochi ya Mzee Ngosha punde alipopokelewa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili alipolazwa kwa ajili ya Matibabu ya kabla mauti hayajamkuta. Mzee
Ngosha alipokelewa katika Hospitali hiyo mnamo tarehe 25 nakufanyiwa vipimo na
kubainika na maradhi ya Kifua na kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkuta
majira ya saa 2:30 usiku wa tarehe 29 2017.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria zoezi la kuaga mwili wa mzee Francis Maige Kanyasu
(Ngosha) anayesaidikiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa wakitoa heshima za
mwisho mbele ya jeneza wakati wa zoezi la kuuaga mwili huo lililofanyika
Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jijini Dar es Salaam. Mwili huo umesafirishwa
kuelekea wilayani Misungwi, Mkoani
Mwanza kwa ajili ya mazishi ambapo msafara umeongozwa na Kamishna Msaidizi wa
Ustawi wa Jamii – Wazee na Walemavu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi. Beatrice Fungamo kwa niaba ya Serikali.
Mkurugenzi wa Idara ya NGO’s kutoka Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Marcel Katemba (kulia)
akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi.
Sihaba Nkinga (hayupo pichani) katika hafla ya kuaga mwili wa mzee Francis
Maige Kanyasu (Ngosha) anayesadikiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa zoezi
lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo.
Wapili kulia kwake ni Daktari Bingwa Magonjwa ya Dharura wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa
(Basata), Godfrey Mungereza aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Harrison Mwakyembe akishiriki kubeba jeneza lililobeba mwili wa mzee
Francis Maige Kanyasu (Ngosha) anayesadikiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa
mara baada ya zoezi la kuuga mwili huo kumalizika katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo. Mwili huo umesafirishwa kuelekea Misungwi
Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Wanahabari, wasanii, watumishi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakibeba jeneza
lililobeba mwili wa mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) anayesadikiwa kuwa
mbunifu wa Nembo ya Taifa mara baada ya zoezi la kuuaga mwili huo kumalizika
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo. Mwili huo
umesafirishwa kuelekea Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Picha
na Frank Shija - MAELEZO
No comments:
Post a Comment