Thursday, June 1, 2017

Milioni 20 za Biko zatua kwa Huruma Mkongwa wa Arusha

DROO ya kwanza ya Sh Milioni 20 na ya kumi kufanywa na waendeshaji wa bahati Nasibu ya Biko hatimae imepata mwenyewe baada ya kutangazwa mshindi wake ambaye ni Huruma Mkongwa wa jijini Arusha, akiibuka kidedea katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.

Droo hiyo ni ongezeko la Sh Milioni 10 ambapo hapo awali droo zote zilikuwa zikihusisha kiasi hicho cha pesa kabla ya kuongezwa katika droo ya Jumatano ambapo waliongeza Milioni 10 nyingine hivyo kufikia Sh Milioni 20 na hivyo kutua kwa Mkongwa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuchezesha droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Jumatano ya Sh Milioni 20 imekuwa tamu baada ya fedha hizo za zawadi ya juu kabisa kutoka kwenda kwa Mkongwa ambapo anakuwa mshindi wa kwanza kuzoa kiasi hicho cha pesa kutoka kwenye bahati nasibu yao inayotikisa nchini.


Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akisalimiana na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid kabla ya kuanza kuchezesha droo ya 10 ya Jumatano ya Sh Milioni 20 ambapo mkazi mwingine wa Arusha, Huruma Mkongwa aliibuka kidedea.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akimtangaza mshindi wa Sh Milioni 20 Huruma Mkongwa kutoka mkoani Arusha baada ya kumaliza kuchezeshwa droo hiyo ya 10 ya Biko. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid.
Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akifurahia jambo baada ya kupatikana mshindi wa Sh Milioni 20 katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam.

Alisema ni imani yao ni kwamba kutoka kwa fedha hizo kutazidi kuibua fursa sahihi kwa washindi wao katika kuhakikisha wanatumia vema fedha hizo ili wanufaike kiuchumi kwa kutumia rasilimali fedha wanazopata kutoka Biko.

“Jumatano ya leo imekuwa Jumatamu kwa mshindi wetu Huruma Mkongwa wa Arusha kupata mkwanja kutoka kwetu, huku Biko tukiwa na lengo kubwa la kukuza uchumi wa wananchi wote hususan wale wanaoamua kutuunga mkono kwa kucheza Biko mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo watakapoingia kwenye lipa bili au lipa kwa Mpesa wataweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.

“Huu ni wakati wa kupata zawadi mbalimbali kutoka Biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambapo hulipwa papo hapo kwa kupitia simu zao walizocheza muda mchache baada ya kushinda, hivyo ili washinde lazima wacheze mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya ushindi,” Alisema Heaven.

Akizungumza kwa simu wakati anafanya mahojiano na Balozi wa Biko Kajala Masanja, Mkongwa alisema haamini kama ameshinda donge nono hilo kutoka Biko ingawa alikiri kucheza Biko akiomba Mungu ashinde ili atimize malengo yake,

“Nashukuru dada Kajala kama mimi ndio mshindi hakika nimefurahi kwa kunitangaza mimi, maana nina uhitaji wa fedha ukizingatia kwamba shughuli zangu kwa sasa nashughulika na mambo ya magari yanayokwenda Namanga,” Alisema Mkongwa.

Naye Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, alisema wanafurahishwa na utaratibu mzima unaofanywa na Biko katika kuwapata washindi wa papo kwa hapo na wale wa droo kubwa ya Sh Milioni 10 na hii ya Milioni 20 iliyofanyika Jumatano na kupatikana Mkongwa kutoka mkoani Arusha.

“Ni wakati wa Watanzania kujitokeza kwa wingi kucheza Biko kwasababu fedha zipo nje nje na kila mtu anaweza kushinda, ukizingatia kuwa Biko wanakidhi vigezo vyote na mchezo wao ni mzuri unaoweza kutoa fedha kwa kila Mtanzania,” Alisema.

Mkongwa anakuwa mtu wa kwanza kushinda donge nono la Sh Milioni 20 lililowekwa katika droo ya Jumatano, huku akiwa mtu wa pili kushinda dau kubwa likiwapo la Sh Milioni 10 ambapo zimetolewa kwa washindi tisa, huku yeye pekee akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake Sh Milioni 20 mapema iwezekanavyo kama atakavyopewa utaratibu na Biko.

No comments:

Post a Comment