Monday, June 12, 2017

Mbio za mwenge wa uhuru zazindua ujenzi wa kiwanja cha Philip Morris Tanzania mjini Morogoro


Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania Ltd Dagmara Piasecka akipokea mbio za mwenge wa Uhuru baada ya kuzindua ujenzi wa kiwanda mjini Morogoro Jumamosi .
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro. Ujenzi wa kiwanda hicho ambao utagharimu zaidi ya 60bn/- utawaongezea faida wakulima wa zao la tumbaku hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka. 
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka.
 

Wakulima wa zao la tumbaku nchini wanatarajia kufaika na ulimaji wa zao hilo baada ya kampuni yaPhilp Morris Tanzania Limited kuwekeza zaid ya Sh. Bilioni 60 kwenye ujenzi wa kiwanda kipya, eneo la Kingolwira katika Halmashauri ya Morogoro mjini.

Kampuni ya Philip Morris ambayo imekuwa ni mnunuzi mkubwa zaid wa tumbaku inayolimwa zaidi hapa nchini ikiwa inanunua zaidi ya asilimia 40, inatarajiwa kuongeza ununuzi wake baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda.

Akiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho, kiongozi wa kitaifa wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema amefurahisha na uamuzi wa kampuni ya Philip Morris Tanzania kuamua kujenge kiwanda hapa nchini kwani mbali na kuongeza ununuzi wa zao la tumbaku na kuongeza kipato kwa wakulima wetu, lakini pia kitatoa ajira kwa watanzania na pia kuongeza na kukuza uchumi wa taifa.

‘Nimepata taarifa kuwa kampuni hii imekuwa ndio inaongoza kwa kununua tumbaku ya Tanzania na sasa mmeamua kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Nawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambapo kauli mbiu yake ni Tanzania ya viwanda. 
 
Lakini pia serikali imekuwa kwa muda mrefu ikitaka makampuni kuwekeza kwenye viwada na hasa vya mazao ya kilimo kwa kunaongeza thamani ya mazao yetu na kuongeza kipato kwa wakulima wetu,’ alisema Amour huku akiongeza kuwa makampuni mingine yanayonunua bidhaa za mkulima ni muhimu wakawekeza kwenye viwanda ili kupata bidhaa za mwisho zinazotengenezwa hapa nchi.

Serikali imekuwa msitari wa mbele kuunga juhudi zozote za kuinua kipato cha wakulima wetu. Hii imejidhiirisha baada ya budget ya mwaka kufuta baadhi ya kodi ambazo zimekuwa ni changamoto kwa wakulima. Hii yote inaonyesha ni jinsi ngani tumekuwa msitari wa mbele kukuza sekta hii kwa vyovyote mwekezaji yeyote inakuja na kuwekeza kwenye kilimo ni wa kupongezwa, aliongeza Amour.

Nawapa changamoto wakulima wetu wa tumbaku kuongeza bidii ya kulima zao hilo kwani mnunuzi mkubwa wa zao lao kwa sasa ameamua kuja na kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Hii ni faida kwa upande wao. 


Aliongeza Amour huku akitoa rai kwa wafanyikazi ambao watapata ajira kwenye kiwanda hicho cha Philip Morris Tanzania kufanya kazi kwa bidii kwani kutakuwa ni chachu ya kuvuta wawekezaji zaidi.’Uwekezaji kama huu ni taji kwa wasomi wetu kwani kunapanua ajira hapa nchini lakini nawaomba Watanzania ambao watapata hiyo fursa kuheshimu kanuni za ajira na kuwa na uhusiano mwema na wawekezaji kwani kiwanda kikifanya kazi zake kwa faida wafanyakazi pia nao watanufaika, alisema Amour.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano Philip Morris Tanzania Evans Mlelwa amesema uamuzi wa kampuni yake kuamua kujenga kiwanda hapa nchini kunatokana na mazingira mazuri ya biashara, amani na utulivu, kiwango cha ukuaji wa uchumi pamoja na sera nzuri ya viwanda hapa nchini  Tanzania.

‘Manufaa ya kiwanda hiki ni katika kuongeza mapato yatokanayo na na kodi kwa serikali, kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na pia kuongeza kwa ulimaji wa zao la tumbaku na kutoa ajira katika nyanja mbali mbali kama uzalishaji na usambazaji, alisema Mlelwa huku akiongeza kuwa kampuni yake itajikita zaidi kwenye huduma za jamii kama elimu na kuhahakisha Wananchi wanaozunguka kiwanda wanapata maji salama kwa matumizi ya nyumbani.

‘Wanawake wamekuwa wakisahaulika sana. Sisi tuna mpango mzuri wa kuwawezesha na kuwainua kichumi na ndio maana nasema kiwanda kiwanda hiki kitakapokamililika kitakuwa na manufaa mengi kwa Wananchi wetu, alisema Mlelwa.

No comments:

Post a Comment