Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza
Baadhi
ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini
hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
Baadhi
ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini
hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina kwa Wastaafu Watarajiwa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akionyesha Vitabu vya PSPF kwenye kutoa elimu kwa Wanachama wa mfuko
huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu kabla ya
ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Benki Kuu jijini Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewaagiza waajira wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama
kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria
ili kukomesha tabia hiyo.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo 3-June-2017 Jijini Mwanza wakati anafungua
semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao,uwekezaji
iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa
ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria
kwenye mifuko hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na
kwa wakati.
Kuhusu
madeni ya Serikali kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini, Makamu wa
Rais amewahakikishia Wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali
inashughulikia madeni hayo na baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki
wa madeni hayo basi malipo yatafanyika haraka iwezekanavyo.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha michango ya
pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zinazopata ruzuku kutoka Serikalini
inalipwa kwenye mifuko hiyo kwa wakati.Aidha, Makamu wa Rais Mhe Samia
Suluhu Hassan amewahimiza wastaafu watarajiwa kote nchini waache tabia
ya kukata tamaa baada ya kustaafu bali wajipange vyema na kuwekeza
katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda vidogo, kilimo na
biashara.
Amesema
kuwa kama wastaafu hao watawekeza katika maeneo hayo watatoa ajira
kubwa kwa vijana badala ya kutumia mafao yao kwenye matumizi yasiyo ya
lazima.
“Wazee
ni rasilimali na hazina kubwa kwa taifa kama waswahili wasemavyo panapo
wazee hapaharibiki jambo hivyo basi ni matumaini yangu kuwa mfuko wa
PSPF mtaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu kuhakikisha kuwa
hazina hii ya wazee wetu wanapata haki zao kwa mujihu wa sheria za nchi
pale wanapohitaji huduma toka kwenu.”Amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameonya wastaafu hao watarajiwa
kupunguza matumizi yasiyo ya lazima bali watumie fedha watakazopata
katika shughuli za kiuchumi kwa ajili ya maslahi yao ya baadaye.Makamu
wa Rais pia amepongeza jitihada zinazofanywa na mfuko wa PSPF kwa kutoa
mafunzo kwa wastaafu watarajiwa kwa ajili ya kuwasaidia kujipanga vyema
pindi watakapostaafu utumishi wao.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji
amewahakikishia wastaafu hao watarajiwa kuwa wa mkoa wa Mwanza kuwa
Serikali itaendelea kusimamia vyema mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze
kutoa mafao bora na kwa wakati.
Dkt Ashatu Kijaji pia amehimiza wastaafu hao watarajiwa kutumia vizuri mafao wanayopata kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
No comments:
Post a Comment