Friday, June 16, 2017

Magreth Sinyangwa wa Kilosa Morogoro apokea Milioni 20 za Biko

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MJASIRIAMALI mwanamke mwenye umri wa miaka 26, Magreth Sinyangwa amekabidhiwa jumla ya Sh Milioni 20 za ushindi wa bahati nasibu ya Biko, aliyoupata katika droo kubwa iliyochezeshwa juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam, huku akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na ushindi huo.

Sinyangwa amekabidhiwa fedha hizo Kilosa katika benki ya NMB, mkoani Morogoro na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ambaye pamoja na mambo mengine, alimpongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu pamoja na kuboresha maisha yake ya kila siku.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Heaven alisema ni wakati wa kutajirika kwa kutumia vyema bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyozidi kuchanja mbuga na kutoa mamilioni ya Sh kwa washindi wa droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili, sanjari na zawadi za papo kwa hapo.


“Tunajivunia kumpata mshindi mwanamke ambaye leo (jana) tumemkabidhi zawadi yake ya Sh Milioni 20, tukiamini kuwa atazitumia vizuri katika kuhakikisha kwamba anakuza biashara zake, ukizingatia kuwa tayari yupo kwenye tasnia ya biashara kabla ya kupata donge nono la Biko.


“Kucheza ni rahisi kwa sababu Biko inachezwa kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo mtu atafanya muamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo ataweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku mbali na donge nono la Sh Milioni 20 linatoka kila Jumatano na Jumapili, pia zipo zawadi za papo hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni,” Alisema Heaven.


Naye Sinyangwa alishindwa kuzuia furaha yake baada ya kukabidhiwa fedha zake, akisema kuwa ameshukuru ushindi wake huo akisema maisha yake yatabadilika kwa sababu atatumia biashara zake zipanuke kwa kutumia vyema ushindi huo wa Biko uliompatia mamilioni ya fedha.


“Huu ni wakati wa kusonga mbele kiuchumi kwa kutumia fedha hizi ambazo nimezipata bila kutarajia, hivyo nawaomba akina mama wenzangu pamoja na Watanzania wote kucheza Biko kwa sababu kila mtu anaweza kushinda bila kuangalia yupo wapi na anaishi vipi.


“Mimi nipo Kilosa Morogoro, lakini nilishangaa nilipopigiwa simu na mtu anayeitwa Kajala Masanja na kuniambia kuwa nimeshinda Biko, lakini nzuri zaidi leo (jana) wameniletea fedha zangu hadi ninapoishi jambo ambalo naona si la kawaida na ni la pekee kwa hawa Biko,” Alisema.


Mbali na kukabidhiwa fedha hizo jumla ya Sh Milioni 20, Biko pia tayari wametoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa washindi wake walioshinda katika mwezi Mei pekee, ikiwa ni siku chache tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu hiyo inayotikisa katika kona mbalimbali hapa nchini.
.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wao wa Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa aliyeibuka kidedea katika droo kubwa iliyofanyika Jumatano iliyopita. Kushoto ni mume wa Magreth, Bahati Ramadhani na mwingine ni Ofisa wa NMB Tawi la Kilosa, akiwa kwenye makabidhiano hayo.
Mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa kutoka kwa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kushoto akiwa ameshika hundi tayari kwa kumkabidhi mshindi wao wa Sh Milioni 20 wa Kilosa Morogoro, Magreth Senyangwa, wa pili kutoka kushoto akifuatiwa na mumewe Bahati Ramadhan pamoja na familia yao.
Mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Biko, Magreth Senyangwa, akiwa amebeba fedha zake mara baada ya kukabidhiwa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wao wa Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa aliyeibuka kidedea katika droo kubwa iliyofanyika Jumatano iliyopita. Kushoto ni Ofisa wa NMB Tawi la Kilosa, akiwa kwenye makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment