Monday, June 5, 2017

Dau nono la Milioni 10 za Biko laenda kwa Junior Pesambili wa Makete

DAU nono la Sh Milioni 10 linalotolewa kama zawadi ya droo kubwa ya Mchezo wa Kubahatisha wa Biko limeenda kwa Junior Ashery Pesambili wa Lupela, Makete, mkoani Njombe, ikiwa ni mwendelezo wa kugawa fedha kwa washindi wake ikitokana na matokeo ya droo ya 11 iliyochezeshwa jana Jumapili.

Droo hiyo iliyochezeshwa jana iliendeshwa na Balozi wa Biko Kajala Masanja, akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Akizungumza katika droo hiyo jana, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema wamedhamiria kugawa mamilioni kwa washindi wao wanaocheza mchezo wa Biko uliozidi kushika kasi katika kona mbalimbali nchini Tanzania.
Alisema tayari wameshafanya droo 11 kubwa ambapo watu mbalimbali wameendelea kupokea fedha zao ikihusisha vijana bila kusahau mzee Stanley Kapondo naye aliyekuwa miongoni mwa Watanzania waliovuna zawadi mbalimbali kutoka Biko.

“Kucheza Biko mara nyingi zaidi ndio nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, hivyo ni wakati wa Watanzania kucheza mara nyingi ili washinde, ukizingatia kuwa mbali na donge nono la Milioni 10 linalotolewa Jumatano na Jumapili, pia mtu anaweza kushinda zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000, 1,000,000, huku droo ya Jumatano hii ikitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wake kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

“Mchezo wetu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo utakapoingia kwenye kipengele cha Lipa Bili au lipa kwa Mpesa, mshiriki wetu ataingiza namba ya kampuni 505050 na baadaye kuweka namba ya kumbukumbu 2456, huku akianzia kucheza kwa Sh 1000 au zaidi,” Alisema Grace.


Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni ya mshindi wao wa Lupela, Makete,mkoani Njombe, Junior Ashery Pesambili aliyepatikana katika droo ya jana Jumapili. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Balozi wa Biko Kajala Masanja akifurahia namba ya mshindi wa Sh Milioni 10 kutoka Makete, mkoani Njombe, droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, aliwapongeza Biko kwa kuchezesha bahati nasibu inayovutia na inayotoa ushindi mnono kwa kupitia simu za mikononi. “Ni utaratibu mzuri unaofanywa na Biko katika kuchezesha bahati nasibu yao, hivyo sisi watu wa Bodi tunachofanya ni kuangalia kama taratibu na sheria zinafuatwa ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo natoa rai kwa kila Mtanzania kucheza Biko ili waibuke na ushindi,” Alisema Maggid.
Akizungumza kwa simu wakati anatangazwa, mshindi huyo hakusita kuonyesha furaha yake, akisema haamini kama ameshinda Milioni 10 za Biko akiongeza kwamba ni wakati wake kukuza uchumi wake kwa kupitia mchezo wa Biko ambao umekuja na kuboresha kipato chake.

“Nashukuru kutangazwa mshindi wa droo ya 11 ya Biko, ambapo kushinda kwangu naamini ni wakati muafaka sasa wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu Mungu amepanga jambo zuri kwangu,ukizingatia kwa sasa najishughulisha na kazi ya uchanaji wa mbao” Alisema. Baada ya kuibuka na donge hilo, mshindi huyo wa Biko anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo ili aziingize kwenye matumizi yake ya kimaisha kwa ajili ya kuinua kipato chake.

No comments:

Post a Comment