Wednesday, June 28, 2017

BARAZA LA MADIWANI WILAYANI BUHIGWE LAMWONDOA MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO KWA TUHUMA MBALIMBALI ZINAZOMKABIRI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Elisha Bagwanya alievaa suti ya rangi ya Blue 
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya  ya Buhigwe Anosta Nyamoga akiwasilisha taarifa ya tume ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma dhidi ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Baadhi ya Madiwani
 
Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

BARAZA la madiwani halmashauri ya Wilayani Buhigwe limemuondoa rasmi Madarakani aliekuwa Mwenyekiti wa halmashauri, Elisha Bagwanya kufuatia kuthibitishwa kwa tuhuma mbili kati ya saba zilizokuwa zimewasilishwa kwa tume hiyo zikimkabili Mwenyekiti huyo, moja ikiwa ni kutumia vibaya madaraka na kuisababishia hasara halmashauri .

Uamuzi huo umetolewa jana Katika viwanja vya Shule ya msingi Buhigwe mara baada ya madiwani wa baraza hilo kupiga kura ya ndio kuunga mkono taarifa ya kamati ya Mkuu wa Mkoa kigoma Brigedia jeneral Emanuel Maganga, iliyokuwa imebaini ukweli wa tuhuma mbili kati ya saba zilizo wasilishwa na madiwani hao na kumtaka mkurugenzi na Baraza kumuondoa Mwenyekiti huyo ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Anosta Nyamoga alithibutisha k kumuondoa mwenywkiti huyo kwa kutangaza matokeo ya kura 20 za ndio na saba za hapana zilozo pigwa na Madiwani wa Halmashauri hiyo .

Nyamoga alisema mnamo tarehe 25 machi alipokea barua kutoka kwa madiwani 20 wa halmashauri hiyo ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wa halmashauri na kwamujibu wa kanuni Na 4(3) ya kanuni za kudumu za Halmashauri wajumbe wa Mkutano wasiopungua theluthi mbili wanaweza kuomba kuitishwa kwa mkutano kwa lengo la kujadili agenda ya kumuondoa madarakani mwenyekiti wa halmashauri kutokana na sababu zinazotajwa, na tuhuma zilizo tajwa katika barua hiyo ni tuhuma saba na moja wapo ikiwa ni kutumia madaraka ya uongozi vibaya kwa kutumia trekta ya halmashauri kulimia shamba lake.

Alisema tume ya mkuu wa mkoa baada ya kupitia tuhuma zote saba zilizotajwa katika barua hiyo ilibaini tuhuma mbili ni za ukweli na zinamnyima Mwenyekiti huyo sifa za kuwa kiongozi, tuhuma hizo ni pamoja na kufanya kazi ya ukandarasi na halmashauri kwa kutumia kampuni yake inayoitwa BUYENZI GENERAL SUPPLIES kwa kazi ya mradi wa maji Nyamugali ambao ni mbovu ,mradi wa Barabara ya Kijiji cha Kigogwe Mrungu kujenga mradi huo kwa kutumia kampuni ya NGELUKE CONSTRUCTIONS kwa kutumia uwezo wake kama mwenyekiti wa halmashauri na kuzuia miradi hiyo isikaguliwe.

Alisema Kuthibitika kwa tuma hizo mbili zinamuondoa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuwa Mwenyekiti na halmashauri hiyo ya Buhigwe inaungana na Mkuu wa Mkoa kumuondoa madarakani kutokana na ukiukwaji wa kanuni alioufanya Mwenyekiti huyo, ilikuhakikisha halmashauri hiyo inapata kiongozi mwingine na inaemdelea na majukumu yake.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marco Gaguti kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa aliwaomba madiwani hao kuweka mbele masilahi ya Wananchi walio wachagua ilikuhakikisha haki inatendeka na halmashauri inakuwa salama kwa kupata Viongozi waadilifu na wanaozingatia maadili ya uwajibikaji na kuwatumikia Wananchi.

Kwaupande wake aliekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elisha Bagwanya alisema yeye kwaupande wake alijitoa katika kampuni ya BUYENZI GENERAL SUPPLIES tangu mwaka 2011 na katika tuhuma hizo saba hakuna tuhuma hata moja inayo muhusu , kuanzia alipoingia madarakani hakuwahi kuomba kufanya kazi yoyote katika halmashauri hiyo na haoni sababu ya yeyekuondolewa katika nafasi yake.

Alisema tatizo linalojitokeza ni baadhi ya madiwani wenzake kuwa na uchu wa madaraka na kupanga kumiondoa katika nafasi yake na kwamba yeye hanatatizo loloye na anastahili na

Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo mara baaada ya kupokea taarifa ya tume ya Mkuu wa Mkoa waliionyesha kutolizishwa na uamuzi huo na baadhi a akiwemo diwani wa kata ya Kajana Robisoni Ngeze waliafiki maamuzi hayo , alisema wao wanaunga mkono maamuzi ya Mkuu wa Mkoa na tuhuma hizo ni za kweli tume iliyoundwa haiwezi kusema uongo na hawawezi kuwa na uchu wa madaraka yake na kwamba maazimio yaliyotolewa ni mazuri na yanaungwa Mkono na Baraza.

Alisema Baraza la madiwani linaushahidi na tuhuma hizo kwamba mwenyekiti huyo aliwahi kuwaomba madiwani wasiende kukagua mradi huo wa Maji na barabara awapatie fedha na madiwani waligoma na kudai lazima miradi hoyo ikaguliwe, tuhuma hiyo inatosha kiwa mwenyekiti huyo hafai kuwa katika kiti hiko.

Hata hivyo mwenyekiti ya tume ya uchunguzi ya tuhuma zinazo mkabili Mwenyekiti wa halmashauri Moses Msuluzya alisema tume ilichunguza na kubaini tuhumba mbili kati ya saba zilizo wasilishwa na madiwani, alisema mwenyekiti aliandika barua ya kuondoka katika kampuni hiyo na mwaka 2015 aliandika barua kwa siri ya kuomba kurudi katika kampuni, na baada ya kustaafu udiwani aliomba fedha yake ya kiinua mgongo iingizwe katika kampuni ya Buyenzi na kudai yeye ndiye mtia saini pekee katika kampuni hiyo.

Alisema vielelezo hivyo vilitosha kuonyesha kuwa tuhuma hizo ni kweli na hapaswi kiendelea kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani wameamua kumuondoa na halmashauri itaendelea na mchakato wa kumpata mwenyekiti atake wajali na kuwatetea wananchi bila kujali maslahi yake.

Wananchi wa halmashauri hiyo, akiwemo mzee Yasini Kandaga alisema anawashukuru sana madiwani kwa kuamua kumuondoa Mwenyekiti huuo, alikuwa akitumia madaraka yake vibaya na kupelekea kuzolotesha maendeleo ya wilaya hiyo na kuwanyanyasa wananchi kutokana na uongozi aliokuwanao.

Alisema serikali ya sasa ni serikali inayowajali wananchi nakuwaomba madiwani kutenda haki na kuchagua mwenyekiti mwingine ambae ni mwadirifu na atakae kuwa na maono ya kuibua miradi itakayo weza kuinua uchumi wa Wananchi wa Wilaya hiyo

No comments:

Post a Comment