Wednesday, June 14, 2017

ABIRIA WA FAST JET WAKWAMA KWA ZAIDI YA SAA SITA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA JNA NA KUSHINDWA KUSAFIRI KWENDA MBEYA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Abiria wa Shirika la Ndege la Fastjet wameshindwa kusafiri kwende mkoani mbeya kutokana na ndege hiyo kushindwa kuruka kwa kukosa kifaa cha kuwasha na kuzimia ndege katika uwanja wa kimataifa wa Songwe.
Globu ya Jamii ilifika katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kukuta abiria wakiangaika bila ya kuwa na msaada mbadala wa safari yao na kuzunguma nao ndipo abiria mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sylvester Lwila akaamua kueleza kuwa wamekaa hapo uwanjani kuanzia saa sita na nusu mpaka saa mbili usiku bila ya mafanikio ya Safari.
"nimekuja hapa uwanjani saa sita tuka Board vizuri tu na kukaa ndani ya ndege kwa zaidi ya saa moja lakini baadae tukaletewa tangazo kuwa tutoke nje ya ndege na mizigo yetu ndege imepata itilafu hivyo inafanyiwa matengenezo kisha baadae tutaingia itaruka ndipo wote tukatoka"anasema Lwila.
anasema kuwa wamekaa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa sita bila mafanikio hivyo wakamua kuanza kudai nauli zao lakini mmoja wafanyakazi wa shirika hili akatuambia hawawezi kurudisha nauli leo hivyo wanatupeleka kulala katika moja ya hoteli iliyopo katika maeneo ya tabata.
hata hivyo mpaka Globu ya jamii inaondoka uwanjani hapo kulibakia abiria watatu ambao waligoma kwenda kulala katika hoteli hiyo wakitaka wapewe pesa zao.
hata hivyo Globu ya Jamii ilifanya jitihada za kumtafuta afisa uhusiano na Masoko wa Fastjet,Lucy Mbogoro aliweza kuthibitisha kuwa ndege hiyo imepata itilafu ya kifaa cha kuwasha na kuzimia ndege katika kiwanja cha Songwe mkoani Mbeya hivyo  aitaweza kusafiri mpaka siku ya Alhamisi ambapo kifaa hicho kitakapokuwa kimenunuliwa kutoka nje ya nchi.
amesema kuwa kwa sasa ni vigumu kutaja lini ndege hiyo itaweza kusafiri kwenda mbeya hivyo abiria wote waliokata tiketi za awali watarudishiwa na kuharishiwa safari zao.

 Sehemu ya abiria wa shirika la ndege la Fastjet wakiwa wamekwama na kuduwa katika ofsi za Fastjet zilizopo katika uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya abiria hao kukwama kushindwa kusafiri kwenda mbey kutokana ndege hiyo kukosa kifaa cha kuwashia na kuzimia ndege katika uwanja wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya hali iliyo walzimu abiria hao kupelekwa kulazwakatika moja ya nyumba za wageni zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam.
           
 Meneja wa huduma wa Fastjet akiwa ameshika kiuono mara baada ya abiri kumtka awarudishie nauli na kugoma kuondoka uwanjani hapo
 Mmoja wa abiria akiwa ameketi chini akiwa amechoka mara baada ya kushindwa kusafiri kwenda mbeya na ndege ya Fastjet
 Abiria akiwa ameendelea na kufanya kazi mara baada ya kushindwa kusafiri kwenda Mbeya na shirika la ndege la FastJet
Sehemu ya abiria waliokwama kutokana na kushindwa kusafiri kutokana na ndege hiyo kukosa kifaa cha kuwasha na kuzimia ndege katika uwanja wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya

No comments:

Post a Comment