Friday, May 5, 2017

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (katikati), akipokea funguo za Magari aina ya Toyota Land Cruiser  kutoka kwa  Balozi wa Omani hapa nchini, Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam leo. Baada ya kukabidhiwa magari hayo yenye thamani ya takriban milioni 400 za Tanzania, Waziri Mahiga alisema kuwa msaada huo umetolewa na Serikali ya Oman kwa ajili ya kusaidia masuala ya usafiri katika kipindi hiki cha mpito ambapo Serikali inahamia Dodoma. 
Waziri Mahiga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali na Wizara yake kwa ujumla mara baada ya kupokea msaada huo. 
Waziri akiendelea kuongea huku Watumishi wa Wizara yake wakimsikiliza kwa makini.
Balozi Al Mahruqi naye akizungumza na kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano anaoumpata kwenye utendaji kazi wake hapa nchini. Alisema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii.
Sehemu ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika,  Bw. Suleiman Salehe; Mhasibu Mkuu, Bw. Paul Kabale; Kainu Nkurugenzi Msaidizi wa Diaspora, Bi. Tagie Mwakawago  na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga,

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mahiga na Balozi wa Oman
Sehemu ya Madereva wa Wizara nao walihudhuria shughuli hiyo ikiwa wao ndio waendeshaji wa Magari hayo.
Sehemu nyingine ya watumishi na wageni waliohudhuria shughuli hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala akimkabidhi funguo za magari Afisa Usafirishaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Mkenda

Picha ya pamoja mara baada ya shughuli kumalizika.

No comments:

Post a Comment