Monday, May 29, 2017

WABUNGE WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUWASAIDIA WASICHANA WANAOPATA MIMBA SHULENI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 

Mtandao wa Mashirika yanayopinga ndoa za utotoni wameitaka serikali kuweka mfumo madhubuti utakaowawezesha wanafuzni wa kike kuendelea kufurahia haki yao ya kupata elimu bora mara baada ya kujifungua.

Akitoa tamko hilo Mwenyekiti wa mtandao huo, Valerian Msoka amesema Serikali ,wabunge na wadau wengine kujikita katika kupambana na changamoto zinazopelekea mimba za utotoni ikiwemo ubovu wa miundombinu ya elimu kukosekana kwa elimu bora ya afya ya uzazi.

“Mtandao wa kupinga ndoa za utotoni unaamini kuwa Tanzania ina uongozi na wawakilishi wanaojali maslahi ya wananchi ambapo watoto wa kike ni miongoni mwa hao . Na ni kwa sababu hiyo mtandao una imani kuwa sauti yao itsikilizwa kwani wasichana hawa wanaopoteza masomo kutokana na mimba ni sehemu ya nguvu kazi muhimu ya msingi na yenye tija kufikia Tanzania ya Viwanda” amesema Msoka.

Msoka amemaliza kwa kusema kuwa utafiti wa kitaifa kuhusu Vichocheo na madhara ya ndoa za utotoni nchini Tanzania uliofanywa mwaka 2016 umebaini kuwa wasichana wana uelewa mdogo juu ya afya ya uzazi.

Mwenyekiti wa Mtandao wa kutetea wadada wadogo, Valerian Msoka 
Mwenyekiti wa Tamwa , Eda Sanga akizungumza juu ya kuwaomba wabunge kutunga sheria kuwasaidia watoto wanaopata mimba mashuleni 
Mkurugenzi wa Tawla nchini ,Tike Mwambipile akizungumza wakati wa kutoa tamko hilo .
Mkurugenzi wa Shirika la Watoto, Koshuma Mtengeti akizungumza juu ya tamko hilo
Waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo 
Baadhi ya wanachama wa tasisi mbalimbali zisizo za kiserikali wakiwa katika mkutano huo
Waandishi na wana harakati wakisikiliza tamko hilo kwa makini 

No comments:

Post a Comment