Thursday, May 4, 2017

MAVUNDE:VIJANA MILIONI 4 KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA VITENDO


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa vitendo kutoka Kwa Chama Cha Waajiri nchini ATE kwa kushulikiana na Shirika la Kazi Duniani ILO leojijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akionyesha Vitabu vya programu vya mafunzo kwa vitendo mara baada ya kuzindua programu hiyo katika ukumbi wa Hyatt Kempiski leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akikata utepe kuashiria uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Chama cha Waajiri nchini ATE, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa ATE nchini , Almas Maige(MB) akishuhudia uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la kazi Duniani (ILO) ukanda wa Afrika Mashariki ,Dk Mary Kawar akizungumza wakati wa ufunguzi proamu hiyo
Katibu Mtendaji wa ATE ,DK.Aggrey Mlimuka akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa Vitendo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waajiri nchini (ATE), Almas Maige(MB) akichangia jambo katika mkutano huo uliowashirikisha wadau mbalimbali iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mstaafu wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Mhandisi Zebadiah Moshi akichangia jambo katika mkutano huo uzinduzi wa program ya vitendo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bridge for Change, Ocheck Msuva akichangia maada katika uzinduzi ya programu ya mafunzo kwa vitendo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Asasi ya kuhamasishaVijana ya Tanzania Zalendo ,Victoria Mwanziva akichangia jambo juu ya umuhimu wa vijana kujifunza kwa vitendo pindi wanapokuwa mashuleni

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa Vitendo kwa Vijana




Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amesema Vijana zaidi ya Milioni Nne nchini watafikiwa na programu ya mafunzo kwa Vitendo ili waweze kuhimili ushindani pindi wanapohitimu vyuo.

Mavunde amesema hayo leo alipokuwa akizindua programu ya mafunzo kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE) kwa kushirikiana na Shirika la kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki.

“Kwenye program hii ya miaka mitano tunakwenda kuwafikia vijana Milioni Nne nchini ambapo katika mwaka huu wa fedha 2017/2018 vijana 27,000 watapewa mafunzo kwa vitendo” amesema Mavunde.

Waziri Mavunde amewashukuru ATE kwa kuungana na serikali katika kusaidia vijana wa kitanzania kuingia katika mpango huo ambao unaondoa pingamizi la kuwataka vijana kuwa na uzoefu hili waajiriwe katika taasisi mbalimbali.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa ATE , Almas Maige amesema mpango huo utawasaidia waajiri kupata wafanyakazi ambao wataweza kuwasaidia kwa uzalishaji bila ya kuchukua muda mrefu kujifunza.

No comments:

Post a Comment