Monday, May 29, 2017

JIWE LA MSINGI LA UENDELEZAJI WA BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE LAWEKWA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE

Na Francis Dande


Mradi wa Ujenzi wa Barabara inayounganisha Daraja la Nyerere na barabara inayotoka Kigamboni hadi Kibada unaotekelezwa kwa ubia kati ya Serikali na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mradi huu wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1.2 unatarajia kukamilika ndani ya kipindi cha miezi sita.






Akizungumza  wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Prof. Godius Kahyarara, amesema kuwa barabara hiyo itakuwa na njia sita pamoja na mzunguko (Round Abaout) wenye vipande vya barabara za mita 500 kwa kila kimoja, barabara hii itakuwa na uwezo wa kupitisha yenye uzito wa tani 55.

'Aliongeza kuwa ili kutekeleza mradi huuNSSF tayari imetenga Shilingi bilioni 21 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu'.

Aidha alisema kuwa kukamilika kwa mradi huu kutasaidia wakazi wa Kigamboni kutumia barabara hii muda wote wa mwaka bila kuathiri mabadiliko ya hali ya hewa. Pia kutasaidia ukuaji wa viwanda kwa kusaidia usafirishaji wa bidhaa na malighafi.

Barabara hiyo inajengwa na mkandarasi anayejenga barabara hii ndiye aliyejenga mradi mkubwa daraja la Nyerere na ameanza kazi toka Mei 26 mwaka huu na anatarajiwa kukamilisha ujenzi huo Novemba 25 mwaka.

Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hizo za kuunganganisha na daraja la Nyerere na barabara ya Kigamboni-Kibada Kigamboni kutatoa fursa kwa wakazi wa eneo la Kigamboni kuwa na usafiri wa uhakika kwa wakati wote.
 Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada  lililowekwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour. (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni. 
  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada yenye urefu wa kilometa 1.2 wakati kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour alipoweka jiwe la Msingi.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour, akizindua wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa mradi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
  Meneja Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Jamal Mruma (kushoto), akibadilishana mawazo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour (wa pili kulia) akiwa ameongozana na Meneja Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Jamal Mruma (kulia), wakati wa uzindua wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Meneja Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Jamal Mruma (kushoto), akibadilishana mawazo Kiongozi wa Mbiuo za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, akisalimiana na mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru, Bahati Mwinuguta.
Baadhi ya viongozi wa dini na taasisi wakiwa katika hafla hiyo.


 Maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya Menejimenti ya NSSF wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa NSSF.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour (katikati) akiwa katoka picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara (kushoto kwake) baada ya kuweka jiwe la Msingi.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha Daraja la Nyerere na barabara inayotoka Kigamboni hadi Kibada.  

No comments:

Post a Comment