Monday, May 1, 2017

CHANGAMOTO ZATAJWA KUWAELEMEA WATUMISHI-MAGRETH SITTA

Rais mstaafu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi(TUCTA) Bi.Magreth Sitta ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kwa sasa watumishi wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya waajiri kutovitambua vyama hivyo.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambapo kwa upande wa kitaifa maadhimisho hayo yamefanyikia mkoani Kilimanjaro.

Bi. Magreth Sitta amesema kuwa, itakuwa ni jambo jema zaidi iwapo kama waajiri watakaa na wafanyakazi wao na kuziangalia changamoto zilizopo ili hata Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizipata aweze kulifikisha suala hilo kwa Spika wa bunge liweze kutizamwa kwa makini ili kupunguza changamoto husika.

Aliendelea kusema, serikali na makampuni binafsi hulipa kwa mwezi mishahara duni ambapo ni ujira mdogo sana kwa siku ikilinganishwa kupanda kwa gharama za maisha.

Amesema kwa sasa ukubwa wa kodi ya mapato kwa wafanyakazi (PAYE) kodi ya mapato inayotozwa na serikali inawalazimisha watumishi wa serikali na sekta binafsi kulipa kodi mara tatu kwa na zaidi.
Miongoni mwa ulipaji wa kodi hizo ni pamoja na ulipaji kupitia mishahara yao ya kila mwezi, kulipa kodi kila wanunuapo bidhaa mbalimbali na ulipaji wa kodi wakati wa kustaafu.

Aliendelea kusema kuwa, tatizo lingine kubwa ni baadhi ya taasisi za umma na za binafsi ambazo zimekuwa zikikwepa kutekeleza sheria za kazi ikiwemo sheria ya ajira na mahusiano kazini sheria Na. 6 ya mwaka 2004.

Amesema sheria hiyo inalenga kuwashirikisha wafanyakazi kupitia mabaraza ya wafanyakazi kupitisha bajeti za taasisi za umma zilizopokelewa Bungeni bila kuzingatia sheria hiyo hali ambayo imepelekea hali kuwa mbaya zaidi kwenye makampuni ya tasisi binafsi na kuiomba serikali iwe mfano mzuri katika kulipa michango ya wafanyakazi katika mifuko iliyopo.
Rais Mstaafu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi ambaye pia ni mgeni rasmi B. Magreth Sitta akizungumza na wafanyakazi wa umma na taasisi binafsi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.
Wanachi wakimsikiliza Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta leo katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
 Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta akikabidhi cheti cha ushiriki kwa Meneja Rasilimali watu wa  Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA),Pius Matagi kwa nimbi ya Mkurugenzi Mkuu leo katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
 Watumishi wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) wakishangilia baada ya mtumishi mwenzao kukabidhiwa cheti cha ushiriki kwa niamba ya Mkurungenzi Mkuu wa shirika hilo kutoka kwa Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta.
 Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbalimbali leo jijini leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wasamalia wema wakiwapatia  huduma ya kwanza  majeruhi marabaada ya kuangukiwa na geti katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.
 Baadhi ya wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD marabaada ya kuangukiwa na geti katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.
 Majeruhi akiwa  kwenye gari la MSD  akiendelea kupewa hudum ya kwanza 

No comments:

Post a Comment