Wednesday, May 3, 2017

BONANZA LA AFYA KWANZA LAFANA JIJINI ARUSHA

 Wa kwanza  kushoto ni mwandaaji wa Bonanza la Afya Kwanza akiwa na timu ya Triple A Club Fc  kabla ya mechi kuanza
(Habari picha na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini )


Timu ya Tigo Fc ikiwa pamoja na timu ya Triple A Club  FC 

 waimbaji wa bendi ya Ricker nest music band wakiwa katika picha ya pamoja na rais wa bendi hiyo alkievaa nyeupe
 Wachezaji wa timu ya Triple A Club FC wakiburudika mara baada ya mechi kuisha
 Waimbaji wa timu ya Ricker Nest music band wakiwa na mmoja wa washabiki wao wa music wao wakifurahi pamoja
 Timu ya Mringaringa ikipiga jalamba  kabla ya kuingia uwanjani
wavuta kamba




 warembo wakifuatilia mpira kwa makini
 timu ya Triple A wakiwa wanapeana mawazo katika kipindi cha mapunziko
 wadau mbalimbali waliouthuria bonanza hilo wakiendelea kupata vinywaji
 mmoja ya wachezaji wa timu ya Triple A Club FC akiwa anatolewa uwanjani na wauguzi mara baada yakuumia wakati akicheza
 Timu ya Tigo Fc ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya Triple A Klabu Fc kuanza
Na Woinde Shizza,Arusha

Timu ya Triple A klabu imelazimika kutoka sara ya bao moja kwa moja na timu ya Tigo FC  katika bonanza la michezo lijulikanalo kwa jina la Afya Kwanza  lililofanyika katika viwanja vya Gymkana jijini  hapa

 Bonanza hilo ambalo ni mara ya kwanza kufanyika limeandaliwa na  mkurugenzi wa Bendi ya Rickernest music band ,bendi ambayo makao makuu yake ni jijini hapa na imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba  pamoja na mpira wa miguu

Akiongelea bonaza hilo muandaaji wa mashindano hayo Denis  Mtedeki   alisema kuwa nia rasmi ya kuandaa bonanza hili ni kuwakutanisha watu mbalimbali  na kufurahi pamoja  pamoja na kushiriki michezo   ,ikiwa kama ni sehemu ya kufanya mazoezi

Alisema kuwa  bonanza hili limeshirikisha jumla ya timu za mipira wa miguu mbili pamoja na timu zingine mbili ambazo zilifanya kazi ya kuvuta kamba,alizitaja timu hizo kuwa ni timu kutoka kampuni ya simu ya Tigo  (Tigo Fc), Olemringaringa FC, Red Apple,Mijada Fc  pamoja na Triple a klabu FC.

 Denis aliongeza kuwa mbali na kushiriki bonanza hili pia wachezaji na washiriki waliouthuria walipata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo kupima presha na kisukari bure.

Aidha aliongeza kuwa bonanza hili alitaishia hapa bali litakuwa likifanyika kila mwisho wa mwezi lengo ikiwa ni kufanya mazoezi ,kuwakutanisha wadau mbambali mbali na kufurahi pamoja


No comments:

Post a Comment