Monday, April 24, 2017

WAUGUZI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WASHEREHEKEA GET TOGETHER PARTY 2017

Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (wa tano kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo Dae es Salaam Jana April 22, 2017. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (wa nne kulia)  akigonganisha Glas zenye kinyaji cha shampeni na Wakuu wa vitengo mbalimbali wa  Hospitali hiyo

Baadhi ya Wakuu wa Idara na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika Gari kuelekea katika kusheherekea sherehe yao iliyofanyika Navy Beach Kigamboni Dar es Salaam jana
Baadhi ya wanakamati wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Segla Mgaya (wa tano kushoto) ambaye ni Afisa Muuguzi wa hospitali hiyo  
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH, Agnes Mtawa  akizungumza na wauguzi hao wakati wa kusheherehekea Get Together Party 2017 iliyofanyika Dar es Salaam jana April 22, katika Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni  ambapo alipata nafasi ya kuanza kutowa  salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo,  Profesa Lawrence Museru kwakutofika,
Mtawa alisema, pokeeni salamkutoka kwa mpendwa wetu Mkurugenzi,  anawasalimia sana na kuwatakia heri katika sherehe hii na amesema Mungu akitupa uzima mwakani anaomba taarifa apate mapema iliaweze kuserebuka nasi na kwakumalizia salamu hizo alisema  pia naomba mpoke salam zake
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (kushoto) akipokea Ua kutoka kwa mtunza hazina wa Kamati hiyo, Matilda Mrina ambaye ni Afisa Mkuu Msaidizi Daraja la Kwanza 
Meneja wa Jengo la Mwaisela, Unyanjite Hema akicheza mchezo wa karata na Muuguzi, Debora Bukuku wakati wa Sherehe hiyo
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa akizindua mchezo wa mazoezi kwa kuruka kamba mbele ya Wauguzi (pichani hawapo) wakati wa kusheherehekea, Get Together Party 2017 iliyofanyika Dar es Salaam jana April 22, 2017 katika Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni , ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ya kuchangamsha mwili ikiwemo, kuruka kamba, kucheza karata, kuogele, kucheza mpira na Burudani ya nyimbo mbalimbali kutoka kwa kikundi cha wasanii cha wauguzi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, michezo hiyo iliyoratibiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Segla Mgaya
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa pili kushoto) akisindikizwa na wauguzi hao na wapilikulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Segla Mgaya


Muuguzi wa Hospitali hiyo, Vaileth Minja akifungua Sherehe hiyo kwa Salaa
Wauguzi wakicheza


Mkurugenzi Agnes Mtwa akicheza pamoja na wauguzi hao
Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa (mwenye mkanda mweusi tumboni) akionyesha umahiri wake kwa kucheza  kwaito na  wauguzi hao

Mwenyekiti wa Kamati hiho, Segla Mgaya  akiwa katika picha ya pamoja na Wauguzi hao
Meneja wa Tawi la Benk NMB Muhimbili, (jina halikupatikana mara moja) akizungumza na wauguzi hao akisisitiza, anaomba kushirikiana na Wauguzi hao, hayo aliyasema wakati wa Sherehe ya Get Together Party 2017, iliyofanyika Dar es Salaam jana katika Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni, alianza kwa kusema, 
Sisi wana wa NMB tunaamini kwa wafanyakazi wanapokutana kwa pamoja wanaongeza ufanisi wa kazi kwa sababu wanakutana pamoja na wanapokuwa Muhimbili kila mmoja anakuwa Bize na kazi yake, lakini hapa mnaweza kubadilisha mawili matatu nakuweza kubadilisha mawazo, alisema
Sisi wana wa NMB tunaimani wafanyakazi wa Muhimbili wana watoto, kwahiyo tumewaletea bidhaa adimu ya mototo Akaunt ambayo unaweza kuifungua pale kwetu katika Tawi letu lililopo Muhimbili, alisema
Ninaimani pale kwetu tunavibanda kama sita ambavyo kuna wahudumu na ukifika pale utamwambia muhudum unahitaji huduma hiyo na atakuletea fom na utaijaza na kingine siolazima kwa wewe kuja Benk kuja kuweka pesa.
Utajazishwa fom ambayo ikifika tarehe ambayo uliambia benk utakumbushwa na ile pesa itatoka kwenye Akaun yako na itakwenda kwenye Akaut Mtoto. alisema Menena huyo.
Huduma hiyo nimbure kabisa kwani kwakufanya hivyo nikuwaandalia watoto wetu msingi bora wa maisha na kuwaandalia ufanisi wao katika masomo yao ya kila siku.
Karibuni sana na ninaomba tuendelee kushirikiana asanteni sana
  
Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa akiwaonyesha zawadi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Segla Mgaya (wa kwanza kulia) iliyo andaliwa wauguzi hao

Afisa Muuguzi, Agnes Kaberege akifungua  Shampeni

Mkurugenzi wa Uuguzi akiwasalimia wauguzi na kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kuwepo mahala hapa kwa siku ya leo,
Mtawa alisema, nijambo la kihistaria mimi tangu niingie kufanya kazi hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili sikumbuki kufanya kitu kama hiki,
Kwakweli nawashukuru kwa kubuni wazo kama hili na kwa sisi tuliyofika hapa na ninajuwa wauguzi tupo wengi lakini niwachache walioitikia wito na ninafikiri huu ni mwanzo mzuri,
Mungu akitupa Uzima wakati mwingine hapa patakuwa hapana nafasi ya kucheza pamoja na mvua nyingi lakini mmeweza kujitowa kwa kuja mahali hapa, alisema Mtawa
Nawaomba nduguzangu Wauguzi tuendelee kuwa na umoja kwa kushikamana kama tulivyoonyesha siku ya leo, tuendelee kupendana, kupeana nguvu kwa sababu kazi yetu kama mnavyo ijuwa kunachangamoto nyingi,
Lakini tukiwa kama mahala kama hapa tunacheza na kufurahi ausio jamani? kwa kuangalia Bahari na yale mabo mengine mengine tumeyaacha getini, kwahiyo pamoja na shukrani nyingi nawaomba tufurahi kwa pamona, alisema Mtawa kwa kumalizia ,
Leo si siku ya hutuba ni siku ya kufurahi 





Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Segla Mgaya (kulia)  akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Mtawa, wanaoshuhudia ni wanakamati
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa nne kulia) walio kaa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Sherehe hiyo
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa nne kulia) walio kaa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Sherehe hiyo
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa tatu kulia) walio kaa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benk ya NMB






No comments:

Post a Comment