Thursday, April 27, 2017

WAKAZI WA TABORA WANAOKWENDA KITETE WAONDOKA NA ADHA YA SEHEMU YA KUKAA

 Tiganya Vincent, RS-Tabora

 Wananchi wa Mkoa wa Tabora wanakwenda kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete wameondokana na adha ya muda mrefu ya kunyeshewa mvua na kukaa juani baada ya kukamilika na kuzinduliwa kwa Jengo la Mahali pa Kungonjea kuona wagonjwa.
 
Jengo hilo lililojengwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora na umegharimu shilingi milioni 18 hadi kukamilika.
 
Uzinduzi huo umefanywa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen Mlozi wakati wa sherehe fupi zilzofanyika katika Hospiali ya Rufaa ya Mkoa huo Kitete.
 
Alisema kuwa kukamilika  kwa jengo hilo kwa muda kumesaidia kuondoa kilio cha muda mrefu cha viongozi na wananchi cha kutaka lijengwe eneo la watu kupumuzika wakati wakisubiri muda wa kuona wagonjwa wao wanapata matibabu katika Hosptali hiyo.

Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliipongeza Seketarieti ya Mkoa wa Tabora kwa kuwa wabuni hadi kufanikisha ujenzi huo kwa kiwango cha juu na gharama nafuu.
 
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefanywa kwa kutumia fedha za usimamizi wa miradi ambapo Seketarieti ya Mkoa huo imepunguza katika fedha zake za kufuatilia miradi.
 
Alisema kuwa hatua hiyo imesaidia kupatikana kwa fedha hizo zilizosaidia kukamilisha kwa jengo ambalo ambalo litasiadia kuepusha wananchi hao na hatari za kugongwa na baiskeli au pikipiki kutokana na kukaa kando kando ya barabara.
 
Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kabla ya ujenzi huo walitaka kumtumia Mhandisi kutoka nje ambapo alidai apatiwe shilingi milioni 35 ili afanikishe ujenzi huo , lakini walipoamua kutumia mwandishi wa ndani wameokoa kiasi cha milioni 17.
 
Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa Wakurugenzi wote Watendaji wa Halmashauri nane(8) za mkoani Tabora kuhakikisha wanajenga jengo kwa kila Hospitali la Mahali pa wananchi kuongejea kuona wagonjwa wao.
 
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwaondelea kero wananchi na kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwajali wanyonge.
 
Aidha , Dkt. Ntara aliwaahidi wananchi kuwa baada ya kukamilika kwa jengo hilo atajitadi kuwanunulia runinga ili wanapokuwa wanasubiri kuona wagonjwa wafutilie taarifa mbalimbali za habari zinaendelea za ndani na nje ya nchi.
 
Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora wanatarajia kujenga Kliniki mbili katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete kwa ajili ya vijana na wakinamama.
 
Alisema kuwa lengo la kutaka kufanya hivyo ni kutaka kutoa elimu kwa vijana hasa mabinti kwa ajili ya kupunguza ndoa na mimba za utotoni mkoani Tabora.
 
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete ilijengwa katika miaka ya 1909 lakini ilikuwa haina sehemu ya watu kukaa wakati wakisiburi kuona wagonjwa.
 

No comments:

Post a Comment