Tuesday, April 4, 2017

UTEUZI WA WAGOMBEA WA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


BUNGE LA TANZANIA
 _________
TAARIFA
____
 KUHUSU

UTEUZI WA WAGOMBEA WA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI
______

1.   Tarehe 17 Machi, 2017 nilitoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali Namba 376 kuhusu Siku ya uteuzi na Siku ya Uchaguzi. Katika Tangazo hilo, nilipanga Siku ya tarehe 30 Machi, 2017, saa Kumi (10.00) Jioni kuwa Siku ya Uteuzi wa Wagombea na pia siku ya tarehe 04 Aprili, 2017 saa Tano (5.00) Asubuhi kuwa Siku ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.

2.   Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote hususan Vyama vyote vya siasa nchini kwa ushirikiano mzuri nilioupata kutoka kwao katika zoezi zima la mchakato wa uteuzi wa wagombea.

3.   Vile vile, navipongeza na kuvishukuru vyama vyote vya siasa vyenye haki ya kushiriki uchaguzi kwa kuendesha mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa uwazi na demokrasia kubwa.

4.   Pia navishukuru vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ujumla kwa kuhabarisha umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa Bunge na Taifa kwa ujumla.

5.   Kipekee nawashukuru na kuwapongeza wananchi wote waliojitokeza kupitia vyama vyao kugombea katika uchaguzi huu ambapo jumla ya Watu 505 walijitokeza kugombea kupitia vyama vifuatavyo:

A.  CCM- Wagombea-471;
B.  CHADEMA- Wagombea-17;
C.  CUF-Wagombea-8;
D.  NCCR-MAGEUZI- Wagombea 3; na
E.   ACT-WAZALENDO-Wagombea-6.

6.   Wagombea hao walichujwa na Vyama vyao na kupata majina ya watu 20 waliopitishwa kugombea kwa mchanganuo ufuatao:

A.  CCM-Wagombea 12;
B.  CHADEMA-Wagombea 2;
C.  CUF-Wagombea-4;
D.  NCCR-MAGEUZI-Mgombea 1; na
E.   ACT-WAZALENDO-Mgombea 1.

7.   Kati ya Wagombea hao Wanaume ni 12 na Wanawake ni 8 kwa Mchanganuo ufuatao:

A.  CCM-Wanawake 6 na Wanaume 6;
B.  CHADEMA- Wanawake 0 na Wanaume 2;
C.  CUF-Mwanamke 1 na Wanaume 3;
D.  NCCR-MAGEUZI-Mwanamke 1 na Wanaume 0; na
E.   ACT-WAZALENDO-Wanawake 0 na Mwanaume 1. 

8.   Majina hayo ya Wagombea yaliwasilishwa na Vyama vyao kwangu tarehe 30 Machi, 2017 kabla ya Saa 10 Jioni kama masharti ya Kanuni ya 5(4) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.

9.   Baada ya hatua hiyo, nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili kujiridhisha na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa mujibu Ibara ya 50 ya Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Sheria ya Uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5(1), (2) na (3) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016. Ufuatao ni Mchanganuo wa maombi ya kugombea katika Makundi ya Uchaguzi:

KUNDI A:   WANAWAKE

NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.     
Ndg. Happiness Elias LUGIKO
KE
CCM
2.     
Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA
KE
CCM


KUNDI B:   ZANZIBAR

NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.     
Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME
ME
CCM
2.     
Ndg. Maryam Ussi YAHYA
KE
CCM
3.     
Ndg. Mohamed Yusuf NUH
ME
CCM
4.     
Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI
KE
CCM

 KUNDI C:  VYAMA VYA UPINZANI

NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.     
Ndg. Ezekia Dibogo WENJE
ME
CHADEMA
2.     
Ndg. Habibu Mohamed MNYAA
ME
CUF
3.     
Ndg. Lawrence Kego MASHA
ME
CHADEMA
4.     
Ndg. Nderakindo Perpetua KESSY
KE
NCCR
5.     
Prof. Kitila MKUMBO
ME
A CT
6.     
Ndg.  Sonia Jumaa MAGOGO
KE
CUF
7.     
Ndg. Thomas D.C MALIMA
ME
CUF
8.     
Ndg.  Twaha Issa TASLIMA
ME
CUF

KUNDI D:   TANZANIA BARA
         
NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.
Ndg. Adam Omari  KIMBISA
ME
CCM
2.
Ndg. Anamringi Issay MACHA
ME
CCM
3.
Ndg. Charles Makongoro NYERERE
ME
CCM
4.
Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE
ME
CCM
5.
Ndg. Fancy Haji NKUHI
KE
CCM
6.
Ndg. Happiness Ngoti MGALULA
KE
CCM

 10.        Matokeo ya uchambuzi wa nyaraka za uteuzi  wa Wagombea zilizowasilishwa na Chama cha Mapinduzi yanaonesha kuwa wagombea wote wamekidhi vigezo na masharti ya uchaguzi. Ifuatayo ni orodha ya Wagombea hao katika makundi waliyoomba kugombea:


I.           WAGOMBEA WALIOKIDHI MASHARTI NA KUTEULIWA

KUNDI A:   WANAWAKE

NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.
Ndg. Happiness Elias LUGIKO
KE
CCM
2.
Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA
KE
CCM


KUNDI B:   ZANZIBAR

NA.
JINA
JNSIA
CHAMA
1.
Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME
ME
CCM
2.
Ndg. Maryam Ussi YAHYA
KE
CCM
3.
Ndg. Mohamed Yusuf NUH
ME
CCM
4.
Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI
KE
CCM

KUNDI D:   TANZANIA BARA
         
NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.
Ndg. Adam Omari KIMBISA
ME
CCM
2.
Ndg. Anamringi Issay MACHA
ME
CCM
3.
Ndg. Charles Makongoro NYERERE
ME
CCM
4.
Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE
ME
CCM
5.
Ndg. Fancy Haji NKUHI
KE
CCM
6.
Ndg. Happiness Ngoti MGALULA
KE
CCM


II.         UTEUZI  WA WAGOMBEA KATIKA KUNDI C -VYAMA VYA UPINZANI

11.           Uteuzi wa Wagombea katika Kundi C (Vyama vya Upinzani) haujafanyika kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwenye nyaraka za uteuzi wa wagombea ambayo yanakiuka masharti ya Ibara ya 50 ya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki ya Mwaka 2011 iliyotungwa na Bunge la Afrika Mashariki. Muhtasari wa mapungufu yaliyobainishwa kwa Vyama husika ni kama ifuatavyo:

1.  CHADEMA
·        Uteuzi haujazingatia jinsia ili kuwezesha utekelezaji wa masharti ya Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (The East African Legislative Assembly Elections Act, 2011) ya angalua theluthi moja (1/3) ya wajumbe 9 ioneshe uwepo wa jinsia zote mbili (at least one third of the elected members shall reflect either gender).
·        Fomu za maombi ya wagombea hazipo.
·        Orodha ya waombaji haipo.
·        Fomu ya matokeo ya kura haipo.


2.  CUF
·        Uteuzi haujazingatia jinsia ili kuwezesha utekelezaji wa masharti ya Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (The East African Legislative Assembly Elections Act, 2011) ya angalua theluthi moja (1/3) ya wajumbe 9 ioneshe uwepo wa jinsia zote mbili (at least one third of the elected members shall reflect either gender).
·        Fomu za Uteuzi wa Wagombea zimewasilishwa na mamlaka mbili tofauti.
·        Wagombea wawili hawana uthibitisho wa Uraia.
·        Fomu ya uthibitisho wa hiari ya kugombea haipo kwa wagombea wote.
·        Orodha ya waombaji haipo kwa Mgombea mmoja.
·        Fomu ya matokeo ya kura kwa wagombea wote haipo.
·        Fomu ya Mahudhurio kwa mgombea mmoja haipo.
  
12.            Mapungufu hayo yamenifanya nishindwe kufanya uteuzi wa Wagombea katika kundi hilo, hivyo nimeviandikia barua vyama vyenye haki ya kugombea katika Kundi hilo kuvitaka kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa na kuwasilisha majina na nyaraka zinazohitajika ofisini kwangu Dodoma Siku ya tarehe 4 Aprili, 2017 kabla ya saa 7:00 Mchana. 

13.           Uteuzi wa Wagombea katika KUNDI C (Vyama vya Upinzani) utafanyika tarehe 4 Aprili, 2017 wakati wowote kuanzia saa saba kamili (7:00) mchana mara baada ya kupokea na kuchambua nyaraka zitakazowasilishwa kwangu na Vyama husika.

14.           Kutokana na matokeo ya uchambuzi huo na kwa kuzingatia masharti ya  Ibara ya 50 ya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Masharti ya Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Kanuni ya 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge na Kanuni ya 5(1)(2) na (3) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 na Mwongozo wa Spika kuhusu Mgawanyo wa Kura zinazotakiwa kupigwa katika kila Kundi, kwa mamlaka niliyopewa kama Msimamizi wa Uchaguzi NATANGAZA na kutoa TAARIFA kwa Umma kwamba, wafuatao ndio waliokidhi vigezo na masharti ya kuteuliwa kugombea Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki uliopangwa kufanyika tarehe 4 Aprili, 2017 kwa mchanganuo ufuatao:

KUNDI A:   WAGOMBEA WANAWAKE

NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.
Ndg. Happiness Elias LUGIKO
KE
CCM
2.
Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA
KE
CCM

 
 KUNDI B:  WAGOMBEA WA ZANZIBAR 

NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.
Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME
ME
CCM
2.
Ndg. Maryam Ussi YAHYA
KE
CCM
3.
Ndg. Mohamed Yusuf NUH
ME
CCM
4.
Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI
KE
CCM

KUNDI D:   WAGOMBEA WA TANZANIA BARA
         
NA.
JINA
JINSIA
CHAMA
1.
Ndg. Adam Omari KIMBISA
ME
CCM
2.
Ndg. Anamringi Issay MACHA
ME
CCM
3.
Ndg. Charles Makongoro NYERERE
ME
CCM
4.
Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE
ME
CCM
5.
Ndg. Fancy Haji NKUHI
KE
CCM
6.
Ndg. Happiness Ngoti MGALULA
KE
CCM
  
Dr. Thomas D. Kashililah
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI

3 Aprili, 2017



No comments:

Post a Comment