Wednesday, April 26, 2017

RAS –TABORA AWATAKA WACHIMBAJI MADINI WA KITUNDA KUJIKINGA NA VVU


Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora(RAS) Dkt. Thea Ntara amewataka Wachimbaji Wadogo wadogo waliopo eneo la Kitunda wilayani Sikonge kuzingatia matumizi mipira ya kufanyia mapenzi(condom) wanapoamua kufanya hivyo ili kujikinga na maambukizi yanayowekusababishia kupata Virusi vya UKIMWI.

Hatua hiyo itasaidia waweze kuendelea kuwa na afya nzuri itakayowasaidia kuishi maisha mengi na kukatiza ndogo zao.
Dkt. Ntara alitoa kauli hiyo jana wilayani Sikonge wakati akitoa pole kuifuatia Maafa ya wachimbaji Saba wa madini katika eneo la Kitunda ambapo sita walikufa kwa kufukiwa na kifusi na mmoja alikufa kwa kukosa hewa.

Alisema kuwa umati wa wachimbaji ulipo katika eneoi hilo ni zaidi ya elfu kumi, hivyo ni vema wakatumia mipira kujikinga na UKIMWI wakati wakifanya mapenzi ili uwepo dhahabu hapo usije ukasababisha tatizo lingine katika jamii hiyo na ile inayowazunguka.

Dkt. Ntara alisema kuwa wachimbaji wengi katika eneo hilo bado wanaumri mdogo hivyo ni vema wakalinda afya zaidi ili wasiweze kutumbukia katika matatizo yatakayokazi maisha yao na kupoteza nguvu kazi ya Taifa ambayo bado inahitajika sana kwa maendeleo ya nchi hii.

Alisema kuwa ni vema wakatumia fursa hiyo ya uwepo wa dhahabu katika eneo hilo kwa kulinda na kuimarisha afya zao na sio kutumia fursa hiyo kutafuta matatizo ambayo wanaweza kujikinga nayo au kuyaepuka.

Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwataka baadhi vijana wenye tabia za kubaki kuachana na tabia hiyo bali wafuate taratibu za maridhiano zaidi ili kuepuka maambukizi mapya ya UKIMWI.

Alisema kuwa mtu anayetumia nguvu mara nyingi akumbuki kujikinga jambo ambalo linaweza kumsababishia yeye au mwenzake matatizo.

Katika hatua nyingine RAS huyo ameaagiza Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri ya Wilaya Sikonge Daktari Mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha wanapeleka kwa wingi mipira ya kiume ya kufanyia mapenzi katika eneo hilo la wachimbaji madini wadogo ili kuwakinga na maambukizi mapya ya VVU.

Alisema kuwa eneo lina wanchi wengi , hivyo ni vema wakapelekewa vifaa vya kujilinda ili waendelee kuwa na afya bora ambazo zitawasaidia wao kujitafutia kipato halali na kuchangia katika ujenzi wa nchi kwa njia mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi.

Dkt. Ntara aliwaagiza pia viongozi hao kupeleka huduma mbalimbali kama vile za kufungua Zahanati, Mtaalamu wa Afya, kufungua Shule ya Awali kwa ajili kukabiliana na wingi wa watu katika eneo hilo ili nao kama walivyo wananchi wapate fursa za huduma za jamii kwa karibu.

Alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wanaelimishwa juu ya kujilinda na magonjwa ya mlipuko kama vile kipundupindu , na pia kuwapa matibabu pindi wanapokuwa na magonjwa mbalimbali kama vile malaria.

Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwataka wachimbaji madini hao kuzingatia usafi ili wasije wakapata maambukizi ya kipindupindu.Alisema kuwa eneo hilo linawananchi wengine endapo usafi usipozingatiwa upo uwekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora amewataka vijana wote walipo katika eneo ambao hawajafanya tohara kufanya hivyo ili kuimarisha afya zao na kujikinga na magonjwa ambayo yanasababisha na wanaume kutofanya hivyo.

Alisema kuwa huduma hizo zinatolewa katika Hospitali nyingi ni vema wakachangamkia fursa hiyo.

No comments:

Post a Comment