Thursday, April 6, 2017

KAMISHNA JENERALI WA MAMLAKA YA MAPATO (TRA) ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kulia alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Mnazi Mmoja mapema leo asubuhi.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliopo mnazi mmoja katika ziara zake baada ya kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli hapo jana.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoji kutoka kulia ni Naibu Kamishna Billy Mwakatage, Kaimu Kamishana Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla, Mhasibu Mkuu Chakala, Kaimu Kamishna wa Operesheni Christom Manyologa na Kamishana Msaidizi Hamadi Muhando wakimfuatilia kwa karibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere hayupo pichani, alipofanya ziara katika Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 06/04/2017
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimfuatilia kwa karibu huku akiandika, Kamishana MKuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere, Kamishna huyo aliambatana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo (kulia) alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo Asubuhi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimpatia zawadi ya Kalamu ya Jeshi yenye namba ya dharura 114, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) mapema leo asubuhi alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimsindikiza Kamishana MKuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) akiondoka Makao Makuu ya Jeshi hilo alipofanya ziara Mapema leo Asubuhi.(Picha Na Konstebo Joyceana Benson)

No comments:

Post a Comment