Sunday, April 30, 2017

Dkt. Harrison Mwakyembe awataka Vijana kutenga muda wao kujisomea Vitabu.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe (kulia) akiwa amepokelewa na Mwandishi wa kitabu cha "Colour of Life", Bi. Ritha Tarimo siku ya uzinduzi wa kitabu hicho leo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. 



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe pamoja na wageni waalikwa wakiangalia video inayoelezea maduhui ya kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo, 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha "Colour of Life"leo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo. 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo pamja na wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA/HABARI NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana kutumia muda wao kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu badala ya kupoteza muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii kwakuwa kusoma vitabu ndiyo msingi mzuri wa elimu.

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Bi. Ritha Tarimo ambapo katika hotuba yake aliyoitoa mbele ya wageni waalikwa amesisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.

Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa, baadhi ya vijana siku hizi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kujisomea, hivyo amewashauri wajifunze kutoka kwa Mwandishi wa Kitabu hicho ili waje kuwa waandishi hodari wa kutegemewa na Taifa.

Sambamba na rai hiyo, Waziri Mwakyembe amempongeza Bi. Ritha Tarimo kwa juhudi zake kubwa na maarifa katika kutunga na kuandika kitabu hicho ambacho amesema kuwa kitabu hicho ni kizuri na kina maudhui mazuri kwa vijana hususani wanafunzi, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkono kwa kukisoma ili jamii ipate kuelimika.

“Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa yeye ametuonyesha Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki niwaambie ukweli kina maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha”, alisema Dkt. Mwakyembe.


Ameongeza kuwa, Serikali inauunga mkono juhudi zake za uandishi wa vitabu vyake na amechukua baadhi ya nakala za kitabu hicho kwa ajili ya kuzipelekeka kwa Waziri husika wa masuala ya Elimu Sayansi na Teknolojia ili kuona namna gani kitabu hicho kinaweza kuisaidia jamii.

Kwa upande wake Mwandishi Ritha Tarimo ameishukuru Serikali kwa kukubali wito wa kukizindua kitabu chake na pia utayari wa Serikali katika kumuunga mkono ili uandishi wake uwe wenye tija kwa jamii ya Watanzania.Ameeleza kwamba, kazi ya uandishi ameinza muda mrefu na leo ameweza kupata nafasi ya kuungwa mkono na Serikali pamoja na Watanzania mbalimbali ikiwemo familia yake na hatimaye kukamilisha kitabu hicho na kukizindua rasmi.

“Nakushukuru Mhe. Waziri kwa kutumia muda wako kuja kukizindua kitabu hiki, nakushukuru sana na sasa naamini ndoto zangu zinatimia, kitabu hiki nimekitengeneza katika umbo dogo ili kiweze kuwavutia watu wengi kwani kina maudhui mazuri kwa vijana na jamii nzima ya Kitanzania”, alisema Ritha.

Kitabu cha Colour of Life ni moja kati ya vitabu saba alivyoandika Mwandishi huyo ambacho pia kimepata fursa ya kuzinduliwa na Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe na kwa mujibu wa mwandishi huyo, kitabu hicho kina maudhui mazuri kwa vijana katika kuwajenga kimaisha.

No comments:

Post a Comment