Monday, April 3, 2017

ASKOFU DKT NDALIMA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUZIDI KUMUOMBEA RAIS DKT MAGUFULI AWAONYA WANAOGEUZA MAKANISA MAJUKWAA YA SIASA

Na MatukiodaimaBlog 
ASKOFU  mkuu  wa kanisa la Pentecote  Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima  amewataka  viongozi wa  dini  nchini  kutumia nyumba  za ibada  kumwombea Rais Dkt John Magufuli na  kuliombea Taifa badala ya kutumia nyumba  hizo kusema kuumbua viongozi  wa  serikali.
Kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli katika  nchi  hii si  ya kubenzwa makanisani na wachunguzaji ama viongozi wengine wa  dini bali ni kazi ambayo inapaswa  kuombewa  zaidi  ili  Taifa  lizidi kubarikiwa.
Askofu  huyo ametoa kauli hiyo jana  wakati wa  uzinduzi wa kanisa hilo  Mtwivila  mjini Iringa pamoja na kumsimika mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Paul Mtakwimwa   ,kuwa hivi  sasa  heshima ya  nyumba  za ibada  imeanza kupoteza uwepo  wa Mungu kutokana na baadhi ya  watu  kutumia  nyumba   za  ibada kama  sehemu ya masengenyo na utapeli jambo  ambalo  si  sahihi.
Alisema  kitendo  cha baadhi ya makanisa nchini kutumiwa na wanasiasa ama vikundi vya  watu  kuishambulia serikali ama  kufanya utapeli  wa fedha  za  waumini wao kwa kuwatoza fedha  kama malipo ya huduma  wanayoitoa si  sahihi na si kazi ya  nyumba  za ibada hasa makanisa.
Pasipo  kutaja majina ya makanisa   yaliyogeuzwa majukwaa ya wanasiasa na baadhi ya  watu  waovu ama yanayofanya utapeli  wa  pesa  kwa  waumini  wake ,alisema  kuwa yamezuka makanisa ambayo kimsingi hayakupaswa  kuitwa makanisa  ili yalipaswa kuwa ni vyama  vya siasa ama nyumba  za  waganga  wa  kienyeji kwa maana ya  wapiga ramli.
“ Baadhi ya makanisa  yamepoteza sifa ya  kuitwa ni makanisa maana  wanafanya  vituko vya ajabu sana  ndani ya madhabahu ya Mungu …wapo  wanaotumiwa na wanasiasa  kueneza siasa makanisani na  kila  siku  wao ni kuwa ni wachonganishi  dhidi ya  serikali na  watu wake na wengine wamegeuka  watabiri wa  uongo na watenda miujuzi hatarishi kwa jamii “

Alisema  kuwa kazi ya viongozi wa  dini  ni  kuhubiri  neon ili  watu  wote  waweze kumjua Mungu na  sio kuhubiri siasa ama  kuifundisha kazi serikali ya  kufanywa wakati si  jukumu la kanisa kuwa  iwapo watu  wote  watamjua  Mungu  watafanya kazi ya kuhudumia  jamii  kwa  kutanguliza  hofu ya  Mungu hivyo  hakutakuwa na ufisadi , wizi ama watumishi  hewa hivyo kazi ya kanisa ni kuwafanya watu waijue kweli na kweli  iwe ndani ya  mioyo yao.
Askofu Dkt   Ndalima  alisema kuwa kanisa   lake  limeenea  nchi nzima na katika mkoa  wa Iringa  wameanzisha makanisa mawili  katika  mji  wa Iringa na Nyololo  wilaya ya  Mufindi ila lengo lao ni  kuhubiri neon la Mungu kwa usahihi na kuepuka kuwa  kanisa la ujanja ujanja  kama  wanavyofanywa baadhi ya  watu  wanaojiita manabii  ila kazi wanayoifanya  ni  sawa na manabii  wa uongo .
Akielezea  kuhusu utendaji kazi wa Rais  Dkt  Magufuli askofu  huyo  alisema kanisa lake  linampongeza kwani hivi sasa nchi imekuwa na utulivu mkubwa na hakuna  tena maandamano ya  vurugu na  kuwa kila wakati makanisa  yake yatatenga mudu  wa  kumuombea Rais na  watendaji  wote wa serikali na kutumia Biblia katika ibada  zake na  sio  kutumia  matukio na kashfa  za  viongozi  kuhubiri kanisani.

Askofu  wa  kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima akifaya maombi
Baadhi ya  waumini  wa kanisa hilo
mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Iringa Paul Mtakwimwa
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalimaakiwaombea  waumini wake na Taifa
Wachungaji wakiwa katika maombi
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima akimsimika mchungaji Paul Mtakimwa na mkewe
Waumini  wakiwa katika maombi maalum

No comments:

Post a Comment