Kamati za maji za visima kumi vya maji katika manispaa ya Singida zimekuwa sababu ya miradi hiyo iliyokamilika kwa asilimia miamoja kutofanya kazi na kuwanufausha wananchi huku ikiwa imegharimu fedha nyingi za serikali na wahisani hasa benki ya dunia.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki hii mara baada ya kukagua miradi hiyo na kujiridhisha kuwa miradi hiyo imekamilika licha ya kutofanya kazi.
Dkt. Nchimbi amesema sababu kubwa ya kutofanya kazi miradi hiyo ni udhaifu wa kamati za maji na wanasiasa katika maeneo ya miradi kutojali shida ya wananchi ya kukosa maji na hivyo kuitelekeza miradi hiyo badala ya kuisimamia.
Amesema lengo la miradi hiyo ni wananchi wapate maji safi na salama kwa umbali usiozidi kilometa nne kama ilivyoagizwa na serikali.
“Katika ukaguzi wangu nimebaini mifumo katika miradi hii ya maji ipo vizuri sana. Baadhi inaendeshwa kwa umeme na mingine kwa mafuta ya dizel. Makubaliano yalikuwa baada ya kukamilika miradi hii iendeshwe na kamati za maji kwa asilimia mia moja”, amesema.
Dkt. Nchimbi amesema wajibu wa kamati hizo ni pamoja na kukusanya fedha zinazotokana na kuuza maji kwa wateja pamoja na matengenezo ya miundombinu ya visima hivyo ili miradi hiyo iwe endelevu.
“Fedha zinazopatikana ndizo zitakazoendesha mradi husika ikiwemo kugharamia matengenezo ya mashine, pampu, miundombinu, kununulia dizel, umeme na kumlipa mhudumu wa mradi. Makubaliano ni miradi ikikamilika inabaki mikononi mwa wananchi kupitia kamati zao za maji. Serikali na wafadhili hawatahusika tena”, amesisitiza Dkt. Nchimbi.
Dkt. Nchimbi amesema serikali na benki ya dunia imegharamia fedha nyingi kwenye miradi hiyo hivyo haiwezi kuendelea kuona miradi inabaki kuwa mapambo badala ya kuwaondolea wananchi kero ya maji.
“Naagiza wananchi wajipange upya chini ya kamati zao wachague jumuiya za watumiaji maji. Kwenye jumuiya hizo za maji wanaweza kuwepo pia wale waliokuwa kwenye kamati za awali za maji. Jumuiya hizi ziwajibike kikamilifu zihakikishe zinapata fedha kutokana na mauzo ya maji ili waendeleze miradi hiyo kwa ufanisi”, amesema Dkt. Nchimbi.
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo amesema kuanzia mei mwaka huu anataka kuona kila wananchi wa manispaa ya Singida,anapata maji safi na salama kwa umbali mfupi.
“Rasilimali maji ni msingi kwa maisha ya viumbe hai wakiwemo binadamu. Maji yakiwepo tena kwa umbali mfupi mambo yote yatakwenda vizuri. Maji yanasaidia kuweka mazingira safi na afya za wananchi zinaboreka. Maji yana mchango mkubwa kwa jamii inayoelekea kwenye Tanzania ya viwanda”, amesema.
Wakati huo huo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa wanatarajia baadhi ya miradi na hasa ile ya umeme kuibinafisha kwenye mamlaka ya maji safi na maji taka (SUWASA) kwa ajili ya kuiendesha. Mingi itaendelea kumilikiwa na wananchi wenyewe.
Awali mhandisi wa maji manispaa ya Singida Max Hassan Kaaya amesema wanaendelea kuelimisha jamii kuwa miradi hiyo ya maji ni mali yao hivyo jukumu la kuiendesha ni lao. Pia wanapaswa kuilinda na kuitunza vizuri.
Naye mkazi wa kijiji cha Mtamaa Hongoa Bunka amesema elimu zaidi itolewe ili kubadilisha fikiri potofu ya baadhi ya wananchi kuwa jukumu la kuendesha miradi ya maji ni la serikali. Wabadilike na kutambua kuwa ni mali yao na wao ndio watakaoiendesha.
Sunday, April 30, 2017
Dkt. Harrison Mwakyembe awataka Vijana kutenga muda wao kujisomea Vitabu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe (kulia) akiwa amepokelewa na Mwandishi wa kitabu cha "Colour of Life", Bi. Ritha Tarimo siku ya uzinduzi wa kitabu hicho leo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe pamoja na wageni waalikwa wakiangalia video inayoelezea maduhui ya kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo, 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha "Colour of Life"leo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo. 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo pamja na wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA/HABARI NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana kutumia muda wao kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu badala ya kupoteza muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii kwakuwa kusoma vitabu ndiyo msingi mzuri wa elimu.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Bi. Ritha Tarimo ambapo katika hotuba yake aliyoitoa mbele ya wageni waalikwa amesisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.
Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa, baadhi ya vijana siku hizi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kujisomea, hivyo amewashauri wajifunze kutoka kwa Mwandishi wa Kitabu hicho ili waje kuwa waandishi hodari wa kutegemewa na Taifa.
Sambamba na rai hiyo, Waziri Mwakyembe amempongeza Bi. Ritha Tarimo kwa juhudi zake kubwa na maarifa katika kutunga na kuandika kitabu hicho ambacho amesema kuwa kitabu hicho ni kizuri na kina maudhui mazuri kwa vijana hususani wanafunzi, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkono kwa kukisoma ili jamii ipate kuelimika.
“Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa yeye ametuonyesha Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki niwaambie ukweli kina maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa, Serikali inauunga mkono juhudi zake za uandishi wa vitabu vyake na amechukua baadhi ya nakala za kitabu hicho kwa ajili ya kuzipelekeka kwa Waziri husika wa masuala ya Elimu Sayansi na Teknolojia ili kuona namna gani kitabu hicho kinaweza kuisaidia jamii.
Kwa upande wake Mwandishi Ritha Tarimo ameishukuru Serikali kwa kukubali wito wa kukizindua kitabu chake na pia utayari wa Serikali katika kumuunga mkono ili uandishi wake uwe wenye tija kwa jamii ya Watanzania.Ameeleza kwamba, kazi ya uandishi ameinza muda mrefu na leo ameweza kupata nafasi ya kuungwa mkono na Serikali pamoja na Watanzania mbalimbali ikiwemo familia yake na hatimaye kukamilisha kitabu hicho na kukizindua rasmi.
“Nakushukuru Mhe. Waziri kwa kutumia muda wako kuja kukizindua kitabu hiki, nakushukuru sana na sasa naamini ndoto zangu zinatimia, kitabu hiki nimekitengeneza katika umbo dogo ili kiweze kuwavutia watu wengi kwani kina maudhui mazuri kwa vijana na jamii nzima ya Kitanzania”, alisema Ritha.
Kitabu cha Colour of Life ni moja kati ya vitabu saba alivyoandika Mwandishi huyo ambacho pia kimepata fursa ya kuzinduliwa na Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe na kwa mujibu wa mwandishi huyo, kitabu hicho kina maudhui mazuri kwa vijana katika kuwajenga kimaisha.
RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitakiana amani na mmoja wa mapadre katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi Mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Ekaristi Takatifu toka kwa Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiungana na waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na watawa katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na waumini wengine wakimsikiliza Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waumini na wananchi baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waumini na wananchi baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa sala maalumu na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadick wakati wa kuhitimisha ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Muhagama, Askofu Mstaafu Evarist Kweka wakipata picha ya pamoja baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo na Askofu Mstaafu Evarist Kweka baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo na Askofu Mstaafu Evarist Kweka na kiongozi mwingine baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo Aprili 30, 2017. PICHA NA IKULU
MBUNGE WA BUKOMBE AWATAKA WANANCHI KUVUNJA MAKUNDI YA VYAMA NA KUWA WAMOJA
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akiwa kwenye Mkutano wa kutatua na kusikiliza Kero za wananchi kijiji cha Bwenda Kata ya Kantente.
Meza Kuuu hakiwepo Mbunge wa Jimbo la Bukombe pamoja na viongozi wa Kijiji cha Bwenda na wa kata ya Kantente.
Wananchi wakitoa kero zao mbele ya Mbunge wa Bukombe.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akikabidhi mpira kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambayo ilikuwa imeombwa na vijana kwaajili ya kujiandaa na Kombe la Dotto Cup
Diwani wa Kata ya Bulangwa Yusuf Mohamedi akielezea wananchi juu ya serikali ambavyo imejipanga kutatua Kero za wananchi juu ya Elimu pamoja na Huduma ya Afya.
Wananchi wa jimbo la Bukombe Mkoani Geita,wametakiwa kuachana na siasa ambazo zinaweza kusababisha kutokuwa wamoja katika kuleta maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la hilo Dotto Biteko wakati akizungumza na wananakijiji wa kijiji cha Bwenda Namba 9 Kata Ya Kantente ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza Kero za wananchi na kutatua changamoto walizo nazo.
Amesema kuwa maendeleo ya sehemu yoyote hile hayawezi kuletwa kwa watu kutokuwa na umoja na upendo.
"Wana Bwenda inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha tuna maliza changamoto za eneo letu, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na kuzorota kwa ufaulu wa wanafunzi na niombe wazazi mshirikiane na walimu kwa kufuatilia kwa ukaribu zaidi maendeleo ya vijana mashuleni" Alisisitiza Dotto .
Hata hivyo ameongezea kuwa kwa vijana wameanza kutenga asilimia kumi ya mapato na tayari vikundi kumi vimekwisha kupatiwa Mkopo na kwamba ameshapata fedha nyingine ambazo ni milioni hamsini na moja kwaajili ya maendeleo na mikopo kwa vijana na wanawake.
Pia amewataka wanakijiji hao kutokuwaogopa viongozi wao na kuwaambia kama wameshindwa kutekeleza majukumu yao ambayo waliyahaidi wakati wakiomba Ridhaa ya kuongoza kwani ni wajibu wao kuakikisha wanawatumikia wananchi ambao waliwaomba kura wakati wa kampeni.
JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOSOMA BEIJING WAADHIMISHA MIAKA 53 YA MUUNGANO
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania wanaosoma Beijing Nchini Husein Mtoro ( katikati) aliyemwakilisha Balozi,aliambatana na Viongozi wote Wakuu akiwemo Makam Mwenyekiti Khamis Ngwali,Katibu Mkuu Ndugu Remidius Emmanuel,Naibu Katibu Mkuu Ndugu Alinanuswe Mwakiluma na Mweka Hazina Ndugu Kulwa Gamba.
Pamoja
nao,Viongozi waasisi wa Umoja huo Ndugu Suleiman Serera na Irenius
Kagashe nao walishiriki sambamba na Viongozi wastaafu wengine akiwemo
Makam Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Kassim Jape,Katibu Mkuu Mstaafu Angelina
Makoye,Mtunza Hazina Mstaafu Lusekelo Gwassa katika maadhimisho ya
muungano yaliyofanyika mapema wiki hii kwa kushriki maonesho ya utalii
na utamaduni.
Baadhi ya watanzania wanaosoma katika chuo cha Beijing nchini China wakiwa katika maonesho ya utamaduni na utalii kama moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania mapema wiki hii.
Wadau wakipozi kwa picha
Maonesho ya utalii na utamaduni yakiendelea Jijini Beijing
Mmoja wa watanzania anayesoma Beijing akipamba maonesho hayo kwa bendera ya Tanzania wakati wa maonesho ya utalii na utamaduni ikiwa ni maadhimisho ya miaka 53 ya Mungano Hafla hizo zilifanyika mapemaa wiki hii.
Picha ya pamoja
Baadhi ya watanzania wanaosoma katika chuo cha Beijing nchini China wakiwa katika maonesho ya utamaduni na utalii kama moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania mapema wiki hii.
Wadau wakipozi kwa picha
Maonesho ya utalii na utamaduni yakiendelea Jijini Beijing
Mmoja wa watanzania anayesoma Beijing akipamba maonesho hayo kwa bendera ya Tanzania wakati wa maonesho ya utalii na utamaduni ikiwa ni maadhimisho ya miaka 53 ya Mungano Hafla hizo zilifanyika mapemaa wiki hii.
Picha ya pamoja
Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania wanaosoma nchini China,wameadhimisha kumbukumbu ya Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kushiriki MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NA UTAMADUNI katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Biashara na Uchumi jijini Beijing.
Akizungumza
kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini China Balozi MBELWA
KAIRUKI,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,ndugu HUSSEIN MTORO aliwaasa
Watanzania hao kudumisha Amani,Mshikamano na kushiriki katika ajenda
muhimu za Taifa ikiwemo,kushiriki katika kukuza soko la Utalii kwa
kutangaza Vivutio vya asili vya nchi yetu,kuhamasisha Watalii wengi wa
kimataifa kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo Tanzania.Pia
Mwenyekiti alifikisha salam za Balozi Mbelwa za kuwatakia kila la heri
Wanafunzi wote walio katika hatua mbalimbali za kukamilisha Tafiti zao
kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.