Thursday, March 2, 2017

Wadau Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wameremeta mjini Songea

Mdau Glory Lwomile akimvisha pete ya ndoa mume wake Odillon Rweyendera wakati wa misa iliyofanyika katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalembo jimbo kuu la Songea mjini Songea,
Mdau Odillon Rweyendera akimvalisha pete  Glory Lwomile wakati wa ibada ya ndoa iliyofanyika katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalemba jimbo kuu la Songea mjini Songea na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza katika ukumbi wa Familia Takatifu Bombambili.
 Bi harusu Glory Lwomile akila mapozi
 Maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakiwa na furaha mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalemba jimbo kuu la Songea mkoani Ruvuma,Bwana harusi ni mfanyakazi wa shirika la umeme nchini Tanesco mkoa wa Ruvuma na Bi Harusi ni Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakigonga cheers wakati wa sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa familia  Takatifu Parokia ya Bombambili iliyotanguliwa na misa ya  ndoa katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea.
 Ndugu na jamaa wakigonga cheers na maharusi  Odillon Rweyendera na Glory Lwolime  wakati wa sherehe ya kuwapongeza katika ukumbi wa Familia Takatifu Bombambili mjini Songea.
 Maharusi wakikata keki.
  Bwana harusi akimlisha kipande cha keki mkewe wakati wa sherehe ya kuwapongeza kama ishara ya upendo baada ya kufunga ndoa yao.
 Viongozi wa kamati ya maandalizi ya harusi ya Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakifuatilia kwa karibu matukio  ya  sherehe ya kuwapongeza maharusi katika ukumbi wa familia Takatifu Bombambili.
 Maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakipokea zawadi kutoka kwa kamati ya maandalizi ya harusi yao.
 Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wakicheza muziki  na maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwolime, kama ishara ya furaha  kwa ndugu zao kufunga ndoa takatifu.
 Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wakicheza muziki  na maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwolime, kama ishara ya furaha  kwa ndugu zao kufunga ndoa takatifu.

No comments:

Post a Comment