Thursday, March 2, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli ameungana na wakristo wa kanisa katoliki la Mtakatifu Petro lililopo Oystabay jijini Dar es Salaam kusali ibaada ya jumatano ya majivu ambayo ni mwanzo wa kipindi cha Kwaresma. https://youtu.be/R-2IINI_QxE

SIMU.TV: Mtu mmoja wilayani Kalambo amefariki dunia baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani humo. https://youtu.be/8oq_6JrF4rU

SIMU.TV: Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kwa kushirikiana na baraza la habari nchini MCT wamezindua kampeni ya mwaka mmoja kuhusu uhuru wa kujieleza na uhuru wa kukusanyika. https://youtu.be/IVYTLE4DXDk

SIMU.TV: Wafanyakazi na wapangaji wa majengo ya eneo la Kamata jijini Dar es Salaam yaliyokua yakimilikiwa na kampuni ya mabasi ya Air Msae na UDA wametolewa nje ya majengo hayo kkutokana na kushindwa kulipa fedha zinazodaiwa na serikali. https://youtu.be/QDhjlJu9RSc

SIMU.TV: Serikali imeombwa kutafuta suluhisho la haraka la upatikanaji wa makaa ya mawe mkoani Ruvuma ambayo yameadimika na kusababisha kufungwa kwa kiwanda cha saruji cha Rhino kilichopo mkoani Tanga. https://youtu.be/CzOcRbcZ6f0

SIMU.TV: Serikali imeanza kusimamia amri ya usitishwaji wa uzalishaji wa pombe kali inayofungwa katika vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba ambapo taasisi zinazohusika leo zimefanya ukaguzi katika kiwanda cha Tanzania Distilleries Limited. https://youtu.be/32IolyMWIHU

SIMU.TV: Mgogoro baina ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani umechukua sura mpya baada ya kubainika wafugaji huingiza mifugo katika vijiji vya wakulima wakisingizia kuwa ni mifugo ya kulipa mahari. https://youtu.be/tiLarQSQZmk

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Italia kuja kujenga viwanda vya kusindika mazao ya mifugo na uvuvi hapa nchini. https://youtu.be/mXpO6ar775Y

SIMU.TV: Wajumbe takribani mia tatu wanatarijiwa kushiki katika kongamano la nne la wabia wa maendeleo ya kilimo ukanda wa kusini litakalo fanyika jijini Dar es Salaam kuanzia wiki ijayo. https://youtu.be/htuOiTqskB4

SIMU.TV: Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga imerejesha matumaini ya kutetea ubingwa huo, baada ya kuifunga Ruvu Shooting mabao mawili kwa bila na kuacha tofauti ya alama mbili dhidi ya vinara wa ligi hiyo timu ya Simba. https://youtu.be/85YdR9GMVTE

SIMU.TV: Mechi za kwanza za ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa  Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza jumapili ijayo ambapo timu kumi na sita zinatarajiwa kushiriki katika ligi hiyo. https://youtu.be/o-Aae3jQTV0

SIMU.TV: Wilaya ya Kigamboni inatarajiwa kufanya Bonanza kubwa la kutambulisha uwepo wa wilaya hiyo ambapo vikundi vya michezo mbalimbali vitashiriki. https://youtu.be/0LOTfvH2bOY

SIMU.TV: Klabu ya Leicester City imeanza mazungumzo na kocha Roy Hodgson ikiwa na juhudi za kumtafuta mbadala wa Claudio Raniel. https://youtu.be/kZwV9u0l9vU

No comments:

Post a Comment