Saturday, March 4, 2017

RC SHINYANGA ATOA MABATI 171 KWA SHULE TATU WILANI KISHAPU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kishapu, Stephen Magoiga akitoa neno la shukurani kwa mkuu wa mkoa.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wakifuatilia mkutano wa hadhara kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wilayani humo
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Ilobi akitoa kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Wananchi wa kijiji cha Ilobi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wakati akizungumza nao kuhusu maendeleo alipofanya ziara ya kikazi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametoa msaada wa mabati 171 kwa shule za msingi tatu wilayani Kishapu mkoani hapa kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa pindi yatakapokamilika ujenzi wake.

Telack alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi, kata ya Mwaweja wilayani hapa alipofanya ziara ya kikazi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero zao.

Katika msaada huo jumla ya shule tatu za Nyenze iliyopo kata ya Idukilo, Mwasubi kata ya Bunambiyu na Ilobi kwenye kata ya Mwaweja zitanufaika na msaada huo wa mabati 57 kila moja.

Akiwa katika ziara hiyo ya kikazi wilayani hapa, Telack aliagiza wazazi wote kijijini hapo wawapeleke watoto wao na kuwaandikisha shuleni ambapo alisisitiza umuhimu wa elimu kwao.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo kwa wazazi ambao watashindwa kuwapeleka watoto wao shuleni watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Alizungumzia umuhimu wa elimu kuwa ni haki ya kila mtoto hivyo wazazi ni wajibu wao kuhakikisha wanawaandikisha shule badala ya kuwaachia mzigo wa kufanya shughuli za shambani au kuwaozesha.

”Watoto siyo mali wala ng’ombe bali ni wenzetu na ni wakombozi tunataka wakuu wa mikoa watoke hapa, tunataka hata rais atoke hapa kijijini hivyo naagiza kila mtoto aende shule, kamateni wazazi ambao watoto wao hawapo shule,” alisema.

Aidha, Telack aliwahimiza wananchi kijijini hapo na wilaya kwa ujumla kutumia fursa ya kulima mazao ya biashara yakiwemo alizeti, na pamba ili wajipatie kipato na kuendesha maisha yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kishapu, Stephen Magoiga alimshukuru mkuu wa mkoa kwa msaada huo wa mabati na kuahidi kuchangia saruji na mbao za kumalizia kuezekea vyumba vya madarasa.

Aliwahimiza wananchi kuendelea na kuchangia shughuli za maendeleo kwa kujenga vyumba vya madarasa hadi kufikia hatua ya boma ambapo halmashauri itamalizia ujenzi huo.

Magoiga alimuahidi mkuu wa mkoa kuwa halmashauri itakamilisha miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa kupitia nguvu za wananchi ambapo alimualika kuizindua rasmi pindi itakapokamilik

No comments:

Post a Comment