Monday, February 27, 2017

WANACHAMA PSPF SASA RASMI KUPATA MIKOPO KUPITIA BENKI YA CRDB

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.

NA K-VIS BLOG
WANACHAMA wa mfuko wa pensheni wa PSPF sasa wataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya CRDB mara baada ya kuzinduliwa kwa  mpango  huo  baina ya taasisi hizo mbili jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mpango huo  , Mkurugenzi Mkuu  wa PSPF, Bw Adam Mayingu , alisema kuwa mpango huo wa kutoa mikopo kwa wanachama ulianza tangu Desemba 2014 kwa kupitia taasisi nyingine za kifedha.
Alisema kuwa PSPF na benki ya CRDB wamekubaliana  kushirikiana katika kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo.Mikopo hiyo ni pamoja na mkopo wa elimu(education loan scheme), mkopo wa kuanzia maisha( startup life loan scheme) na mkopo wa viwanja(Nipo site na PSPF).
Alisema kuwa kwa upande wa mkopo wa elimu , mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yeyote ya elimu .Ngazi hiyo ni  stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi.
Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, alisema mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa na mahitaji yake muhimu  na kwa kutambua hilo, PSPF kwa kushirikiana na CRDB wameanzisha  mpango huu ambapo mwanachama anaruhusiwa kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili awaeze kujipanga na maisha mapya ya ajira.
Kuhusu mkopo wa viwanja  kwa wanachama, alisema  kuwa  huduma hii itawawezesha wanachama wa PSPF kukopa na kumiliki viwanja vya makazi ambavyo vinapataikana  maeneo mbali mbali ya nchi.
“Lengo  kubwa hapa ni kuwawezesha wanachama wa PSPF kumiliki viwanja vya makazi vilivyopimwa iii kuwaepusha dhdi ya ujenzi katika makazi holela, ambayo yamekuwa na gharama kubwa kuliko makazi yaliyopangiliwa”,alisema.
Alifafanua kuwa lengo kubwa la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto  yake ikiwa ni katika masomo kupitia mkopo wa  elimu , ndoto yake nyingine kupitia mkopo wa kuanzia maisha au mkopo wa viwanja.
Hadi kufikia tarehe 17 Mwezi huu idadi ya wanachama walionufaika na mikopo  hiyo na idadi kwenye mabano ni  Elimu  (1,432)), mkopo wa kuanzia maisha ( 847), mkopo wa viwanja (58).
“Kwa kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ina mtandao mkubwa wa matawi hapa nchini tunaamini watanzania wengi watanufaika na mikopo hii na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatakeleza juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha watanzania wengi zaidi wananufaika na huduma mbali mbali za Mifuko ya Hifadhi ya jamii”, alieleza.
Kw a upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei, alisema azma yao ni kuhakikisha kuwa ushirikiano na wadau wanamkomboa kiuchumi mwananchi  hususan mwenye kipato cha chini  kwa kumpatia  mkopo wenye riba ya asilimia 14 tu kwa mwaka. Kuhusu marejesho alisema ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano.
Ushirikiano wetu na PSPF  bado una muendeleo ulio mpana kwani kwa pamoja tunadhamiria hapo baadae kuingiza sokono mikopo kwa ajili ya wastaafu ‘pensioners’.
Alisema mpango huu wa utoaji wa mikopo kw wastaafu una lengo la kuleta faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbali mbali ya kimaisha ikiwamo kulipia gharama za matibabu, ada za shule za watoto au wajukuaa  na kuendesha biashara ndogo ndogo zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya kila siku.
Dk Kimei alifafanua kuwa  nia yao ni kujenga mazingira mazuri kwa wastaafu walio wanachama wa PSPF ili kustaafu kusiogopwe na kuonekana ni mwanzo wa kuanza kwa kipindi cha maisha ya shida yasiyokuwa na  matumaini.
“Tunataka kujenga tabia ya kuwafanya wafanyakazi wanapopata barua za kustaafu wasihuzunike kama ilivyozoeleka”,alidokezaAlisema kuwa mwanachama wa PSPF anayetaka mkopo anatakiwa aende kwenye tawi lolote la benki ya CRDB ililopo karibu naye ili kupata huduma.
 Bw. Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea ushirikiano huo ambao lengo lake  kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo

 Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo

 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akitoa hotuba ya ukaribisho
 Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (katikati), na Msaidizi Mtendaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Bw.Keneth Kasigila, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Wateja wa Mashirika wa CRDB, Bw.Goodluck Nkini, (kushoto), wakati wa hafla hiyo.
 Bw. Mayingu, (kushoto) na Dkt. Kimei, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo
 Viongozi wa juu wa PSPF, wakipiga makofi wakati wa hafla hiyo
 Baadhi ya maafisa wa CRDB waliohudhuria hafla hiyo
 Baadhi ya maafisa wa PSPF
 Baloziwa PSPF, Mrisho Mpoto, (kushoto), akiongoza kuimba wimbo wa taifa
 Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei, (kushoto) na Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto (katikati), wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo
 Baadhi ya maafisa wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo
 Mkurugenzi wa Mipangona Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akitoa neno la shukrani mwishoni mwa hafla hiyo
 Anna Lukando wa kampuni ya Ardhi Plan Limited, yenye ushirikiano na PSPF, akizungumzia jinsi wanachamawa Mfuko huo wanavyoweza kufaidika  naupatikanajiwa viwanja vilivyopimwa kisheria
 Maafisa wa PSPF na CRDB wakifuatilia hafla hiyo
Maafisa wa CRDB

 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango huo, mfanyakazi wa CRDB, Bi. Fausta Urassa


 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS),  mfanyakazi wa CRDB, Bw.Alfred Kessy.
Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS),  mfanyakazi wa CRDB, Bi. Flora Munisi.

Picha ya pamoja ya wanachama wapya wa PSPF na maafisa wa Mfuko huo akiwemo Balozi Mpoto.
Uzinduzi rasmi ukifanyika

No comments:

Post a Comment