Saturday, February 4, 2017

WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI NA HAKI YA KUPATA TAARIFA NA WAJIBU WAO JUU YA SHERIA HIZO

Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakifu  wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja na waandishi wa habari  mkoani Dodoma katika  ukumbi wa Hazina  Ndogo, iliyolenga kuboresha utendaji katika kazi zao.
Mjadala huu umelenga kuwajengea wanahabari uwezowa utendaji wao wa kazi.Waandishi wa habari hao wamejengewa uwezo kuhusu sheria ya huduma zavyombo vya habari ili kuleta ufanisi katika majukumu yao. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
 Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitoa mada kwa wanahabari waliofika kwenye semina iliyokuwa ikihusu utendaji kazi wao wa kila siku.
Wakili wa Mahakama Kuu na Mhariri wa Zamani, James Marenga akitoa mada inayohusisha sheria mbalimbali zinazohusiana na waandishi wa habari na namna ya kufanya kazi bila kuvunja sheria zilizowekwa.
  Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo kwenye semina ya Wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.
 Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akizungumza jambo kwenye semina iliyowakutanisha wanahabari mbalimbali waliokutanishwa na Misa Tanzania ili kujadili changamoto zinazowapata katika kazi zaohasa za bungeni. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kwa watoa mada waliowasilisha mada mbalimbali katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika semina iliyoandaliwa na Misa Tanzania kujadili namna ya kufanyakazi kifanisi katika majukumu yao ya kila siku
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment