Monday, February 27, 2017

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT.ASHATU KIJAJI AFUNGUA TAWI JIPYA LA FIRST NATIONAL BANK JIJINI ARUSHA

Afisa Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akiongea na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo jijini Arusha mwishoni mwa wiki. 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya FNB Tanzania la Arusha huku akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro (wa kwanza kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa FNB, Dave Aitken(wa pili kushoto) na Meya wa Jiji la Arusha, Mh. Calist Bukhai (kulia). 
Meneja wa Tawi la FNB Arusha, Genevieve Massawe akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji jinsi mashine ya kisasa ya kuweka fedha (cash deposit) na kutoa fedha. Mashine hiyo ya kisasa inamuwezesha mtumiaji kuweka fedha zake benki muda wa masaa 24 imewekwa kwenye tawi hilo jipya ili kuwawezesha wananchi kuweka akiba fedha zao muda wowote ule. 
Mshauri wa Huduma kwa Wateja na Mauzo wa FNB Tawi la Arusha, Cecyline Ayo akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo wakati wa uziduzi wa FNB Tawi la Arusha mwishoni mwa wiki. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akimrekebishia kipaza sati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la FNB Tanzania la Arusha mwishoni mwa wiki. 

-- First National Bank (FNB) Tanzania imeendelea kupanua wigo wake kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la PPF Plaza jijini Arusha kwa lengo la kuhudumia ongezeko la idadi ya wateja katika mkoa huo.

 Akizungumza wakati wa ufunguzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Dave Aitken alisema uzinduzi wa tawi la FNB Arusha umelenga kukidhi ongezeko kubwa la wateja na mahitaji ya huduma za kibenki na kifedha katika kanda ya kaskazini. 

“ Uzinduzi wa tawi la Arusha ni sehemu ya mkakati wa uwekezaji endelevu uliolenga kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia ni kwa maslahi ya ukuaji wa haraka wa mkoa wa Arusha ambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania” Aitken alisema tawi la Arusha ni la kumi miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mitandao ya matawi kwa kusudi la kuyafikia maeneo mengi ya nchini.

 “First National Bank (FNB), daima tunafikiria njia ambazo zinaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Arusha litasaidia kuwapatia huduma zote za kibenki wananchi wa mkoa wa Arusha na wanaoishi maeneo jirani kwani maeneo haya yote yamedhiirika kuwa na biashara mbalimbali zinazokua kwa kasi,” alisema Aitken. 

Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa tawi hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema mkoa wa Arusha una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kudhihirisha kuwa mji unakuwa kwa kasi. 

“Tunakaribisha uwepo wa FNB Tanzania Arusha na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha huduma zenu hapa na mikoa mengine,” Alisema Naibu Waziri. Alisema pamoja na utajiri mkubwa wa maliasili na utalii, mkoa wa Arusha umechangia sana katika kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta nyingine za uzalishaji mali na biashara. 

“Arusha ina fursa na hazina kubwa ya rasilimali jambo ambalo limechangia ukuaji wa haraka wa biashara katika sekta zote muhimu za kiuchumi. Ni matumaini yetu uwepo wa FNB katika mji huu utachangia katika kuleta maendeleo ya biashara kupitia ubunifu wa huduma za kibenki,” Kijaji alisema. 

Vile vile Kijaji ameitaka sekta ya fedha nchini zimetakiwa kutoa mikopo inayosaidia wananchi kukuza mitaji yao ambayo kwa sehemu kubwa itawawezesha katika uzalishaji mali na kuongeza pato lao na nchi kwa ujumla. Amesema kuwa serikali haiwezi kufanikiwa kutekeleza sera na mipango yake kwa ufanisi bila kuwepo sekta binafsi hususani sekta ya fedha hivyo kama serikali inathamini sana mchango wa benki hiyo ya FNB ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia wananchi wa Arusha. 

Tawi la Arusha lililopo jengo la PPF Plaza linakuja na bidhaa na huduma mbalimbali zilizobuniwa mahususi kwa ajili ya kuwaongezea tija wateja wa kawaida na wafanyabiashara katika eneo hili la kanda ya kaskazini.

No comments:

Post a Comment